Uzi maalum: Wapenda mazoezi ya viungo tukutane hapa kwa maoni, ushauri, aina za mazoezi, faida zake n.k

Duuu mi hiyo ndio my record break pace kwa 6Km jana nilijitutumua kwa kweli 5:56 Kutoka 5:58 hizo 2 nafikiri unajua ilivo ngumu kupunguza Pace ya nne siji ifikia labda nikimbie 2Km only nitoke mkuku mkuku maana najua pafupi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaaaa najua mziki wa kupunguza pace ulivyo mkuu ila ni kupambana tu with time unajikuta upo na pace nzuri kabisa.
Kwa mfano kama utaamua kukimbia 6Km unaweza ukaanza kwa pace ndogo kwa 2Km za mwanzo kisha ukaongeza pace kwa 2Km zinazofuata halafu ukamaliza kwa pace yako ya kawaida kwa 2Km za mwisho.
Ukishazoea unaongeza umbali tuseme 8Km.
Nazo unazigawanya kwa mafungu ya 2Km.
Unaanza kawaida,inafuata pace kubwa,inakuja kawaida kisha unamaliza na pace kubwa.
Mbeleni huko unazigawanya katika mafungu mawili ya 4Km.
Unaanza kawaida unamalizia na pace kubwa.
Mpaka kufikia kipindi hicho utakuwa ushajua namna ya kujikontrol kwa pumzi na misuli wakati unakimbia.
Cha muhimu ni kukumbuka kwamba huu ni mchakato wa muda mrefu sio suala la mwezi mmoja au miwili.
Kutoka hatua moja kwenda nyengine kunahitaji malengo,uvumilivu na kujitoa.
Eliud Kipchoge anakwambia "No Human Is Limited"...
Hakuna la kumshinda mwanadamu anapoamua!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah leo nimekutana na Dada yuko fit mazoezini, jinsi alivyokimbia umbali mrefu nami nimejikuta
naenda tu bila kuchoka wakati si kawaida yangu.
 
Anhaa! Jitahidi kuanza kidogo kidogo kama push up 10 asubuhi jioni 10
Baada ya siku 3 ongeza idadi ya kupiga push up mfano 15/20
Ni kweli Mkuu mimi nilikuwa napiga 10 x 5 kila asubuhi kwa sasa naona kama sifanyi kitu
Jana na leo nimepiga 10 x 7 bila shaka nitafika 10 x 50
 
Anhaa! Jitahidi kuanza kidogo kidogo kama push up 10 asubuhi jioni 10
Baada ya siku 3 ongeza idadi ya kupiga push up mfano 15/20
Ushauri mzuri mkuu.
Kwa kuongezea ni kwamba anaweza kujiwekea lengo la kuongeza push up 10 kila baada ya wiki.
Kama wiki hii anapiga 10 wiki ijayo akomae apige 20,wiki inayofuata 30 na kuendelea hivyo hivyo.
Mimi nilianza na push up 20 kwa mkupuo moja kisha napiga 10 mara 3 kutimiza 50 kwa siku.
Nimekomaa na kwa sasa napiga 150 kwa siku,huwa naanza na 50 kwa mkupuo wa kwanza.Kisha napiga 40 halafu napiga 30 mara mbili.
Lengo langu nataka niwe napiga 200 kwa siku kwa mikupuo ya 50 mara nne.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sawa mkuu hata Mimi nifanyapo zoezi hua nakuwa na furaha sana shda nikipumzika dah, hua nakoswa amani kabisa.
 
Duuh!
 
Dah leo nimekutana na Dada yuko fit mazoezini, jinsi alivyokimbia umbali mrefu nami nimejikuta
naenda tu bila kuchoka wakati si kawaida yangu.
Ulikuwa motivated.....
hawa viumbe hutuongezea ari/bidii
ukikutana nao kwenye angle yyte Ile
that is nature
 
Hii ni App gan Mkuu unayoitumia?
 
Hongera mkuu naona unakimbiza haswa .Jeshi la marekani limepiga marufuku maafisa wake kwenye kambi za kijeshi ughaibuni kutumia apps zinazorecord details za location umbali etc ( kama ilivyofanya hiyo yako) na kushare kwenye mitandao kama STRAVA..inaonekana kama vile kuna wadukuzi waliweza kuwafatilia wanajeshi kwa mda mrefu na kufahamu patterns zao za mazoezi mfano anaamka saa ngapi.. Anakimbia kupitia njia ipi.. Anakiambiaga umbali gani.. Anakuaga na nani wakati wa mazoezi nk..hapa kwetu sijui kama mambo haya yapo lakini mkuu
Jana na leo katika harakati za kujenga afya...View attachment 1294131View attachment 1294132

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni App gan Mkuu unayoitumia?
Mkuu ameshajibu swali hili anasema inaitwa SAMSUNG HEALTH nilipumzika kutumia smart mwezi wa 3 sasa
lakini leo naenda kuchukua kasmart hata ka laki na nusu kwa ajili hiyo tu.
 
Ahsante sana mkuu.
Mie pangu pakavu tia mchuzi sina hata cha kuficha na maisha yangu haya hahaahaaaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…