Uzi Maaluma kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina

Uzi Maaluma kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,436
Reaction score
4,756
Mambo Yasiwe Mengi;
Huu uzi ni Maalum kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina.

Sasa Hizi Pini za Luhaga Mpina Sifa yake ni Zianze na Mheshimiwa Raisi Sisi Wakazi wa Bado Tunakudai___ Hivyo kama Hao wengine hawakudai sisi Tuletee Pesa maana Tuna mipango mingi ya maendeleo

Weka Pini Hapa Ukitaja Kero yako na Mahali Kero Ilipo.Usiogope Weka Kero zote Mheshimiwa Rais anazisoma na atakupa Jibu.

Oktoba Tunatiki kwa Nani?
 
Wew bi chakunaku si wakazi wa mwza bado tunakudai,ujenzi wa Airport,utanuzi wa barabara ya Mwza shinyanga,kuanzia Mkuyuni had Usagara..
 
Wananchi wa dar tunakudai hujakamilisha hata mradi mmoja.unatapanya fedha hovyo tu.Tunakudai pakubwa sana.nchi nzima tunakudai
 
Mambo Yasiwe Mengi;
Huu uzi ni Maalum kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina.

Sasa Hizi Pini za Luhaga Mpina Sifa yake ni Zianze na Mheshimiwa Raisi Sisi Wakazi wa Bado Tunakudai___ Hivyo kama Hao wengine hawakudai sisi Tuletee Pesa maana Tuna mipango mingi ya maendeleo

Weka Pini Hapa Ukitaja Kero yako na Mahali Kero Ilipo.Usiogope Weka Kero zote Mheshimiwa Rais anazisoma na atakupa Jibu.

Oktoba Tunatiki kwa Nani?
 
Ninashauri uanzishwe Uzi wa kupiga kura majimbo na miradi ambayo Samia anadaiwa kama rais ili tupige kura
 
Wananchi wa mkoa wa Singida tunakudai Barbara za lami:
1. Manyoni,Itigi kwenda Rungwa kufika makongorosi chunya
Daah hiyo bara bara bado ni vumbi niliona Mzee Magu aliitolea sana macho kama Tabora/Mpanda nikajua itakua ishakamilika kwa hawa jamaa zetu kumbe nayo wameitema ila migodi mikubwa ya dhahabu wamechukua ya makongorosi..
 
Jimbo la Bumbuli,Mkoa wa Tanga, tunamdai Barabara za lami Jimbo nzima
 
Mbunge wangu kasema hatumdai kitu, mitano tena na oktoba tunatiki!
 
Wananchi wa Songea Vijijini, tunakudai haya yafuatayo.

1. Bara bara ya lami na yenye kiwango cha kimataifa, sababu ni border.

Bara bara hiyo ni ya Kutoka Songea Mjini hadi Mkenda, kuvukia Msumbiji kupitia Mitomoni.

Wananchi na watumiaji wa bara bara hii wanapata adha kubwa mno na isiyovumililka hasa wakati wa masika,

2. Maji, katika kata ya Muhukuru bara barani na vitongoji vyake, hadi leo hii hakuna maji kabisaa, suala lililopo, wananchi walichimba mitaro, na kununua mabomba, na hiyo ilitokana na shirika la RC wafadhiri walishinikiza wananchi wafanye hivyo na wao wangetoa msaada wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji.

Cha ajabu Mbunge, Jenista Mhagama, aka cancel ule ufadhiri, na kusema atashughurikia yeye binafsi, km kiongozi wa jimbo, lakini toka afanye hivyo, hakuna kilichofanyika had dakika hii, wananchi wanatumia maji ya visima, na hayo maji ni machafu na hatari, na hayafai kwa matumizi ya kiumbe chochote hai.

Je kwanini wasingeachwa wafadhiri wakamilishe mradi wa maji ktk kata hii? Ikiwa yeye mbunge hawezi na hatoweza? Naomba sana hilii litekelezwe kwa haraka iwezekanavyo.

3. Usuluhishi wa migogoro ya Ardhi, kutoka kata ya muhukuru Bara barani, kijiji cha Maniamba, na vitongoji vyake, kumekuwepo na migogoro ya ardhi kati ya wenyeji, na wageni ambao ni jamii ya wafugaji, (wasukuma, Wamasai na wamang'ati), wananchi wanalalama juu ya ardhi yao kuporwa na kutumiwa na hawa wageni, kila wakiomba muongozo na utaratibu wananyimwa haki hiyo, kumbe viongozi, Akiwa Diwani, mwenyekiti wa kijiji, afisa mtendaji, na vitongoji wao ndo wanawauzia hawa wageni maeneo, kinyume na taratibu na sheria.

Wananchi wanahitaji maeneo yao, hivyo wasaidiwe ktk hili.

.......
 
Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha wanakudai,kujengwa Upya Barabara ya Moshi - Arusha ni mashimo matupu.
Mimi sitetei lakini juzi eid nilikwenda MOSHI naona wanatanua kuanzia USA kwenda mbele huwenda wanafanya njia nne
 
Mambo Yasiwe Mengi;
Huu uzi ni Maalum kwa Ajili ya Pini za Luhaga Mpina.

Sasa Hizi Pini za Luhaga Mpina Sifa yake ni Zianze na Mheshimiwa Raisi Sisi Wakazi wa Bado Tunakudai___ Hivyo kama Hao wengine hawakudai sisi Tuletee Pesa maana Tuna mipango mingi ya maendeleo

Weka Pini Hapa Ukitaja Kero yako na Mahali Kero Ilipo.Usiogope Weka Kero zote Mheshimiwa Rais anazisoma na atakupa Jibu.

Oktoba Tunatiki kwa Nani?

Sisi wananchi wa kusini tunasema: . NO REFORMS, NO ELECTION

#Free Lissu#
 
Back
Top Bottom