Wananchi wa Songea Vijijini, tunakudai haya yafuatayo.
1. Bara bara ya lami na yenye kiwango cha kimataifa, sababu ni border.
Bara bara hiyo ni ya Kutoka Songea Mjini hadi Mkenda, kuvukia Msumbiji kupitia Mitomoni.
Wananchi na watumiaji wa bara bara hii wanapata adha kubwa mno na isiyovumililka hasa wakati wa masika,
2. Maji, katika kata ya Muhukuru bara barani na vitongoji vyake, hadi leo hii hakuna maji kabisaa, suala lililopo, wananchi walichimba mitaro, na kununua mabomba, na hiyo ilitokana na shirika la RC wafadhiri walishinikiza wananchi wafanye hivyo na wao wangetoa msaada wa ujenzi wa miundo mbinu ya maji.
Cha ajabu Mbunge, Jenista Mhagama, aka cancel ule ufadhiri, na kusema atashughurikia yeye binafsi, km kiongozi wa jimbo, lakini toka afanye hivyo, hakuna kilichofanyika had dakika hii, wananchi wanatumia maji ya visima, na hayo maji ni machafu na hatari, na hayafai kwa matumizi ya kiumbe chochote hai.
Je kwanini wasingeachwa wafadhiri wakamilishe mradi wa maji ktk kata hii? Ikiwa yeye mbunge hawezi na hatoweza? Naomba sana hilii litekelezwe kwa haraka iwezekanavyo.
3. Usuluhishi wa migogoro ya Ardhi, kutoka kata ya muhukuru Bara barani, kijiji cha Maniamba, na vitongoji vyake, kumekuwepo na migogoro ya ardhi kati ya wenyeji, na wageni ambao ni jamii ya wafugaji, (wasukuma, Wamasai na wamang'ati), wananchi wanalalama juu ya ardhi yao kuporwa na kutumiwa na hawa wageni, kila wakiomba muongozo na utaratibu wananyimwa haki hiyo, kumbe viongozi, Akiwa Diwani, mwenyekiti wa kijiji, afisa mtendaji, na vitongoji wao ndo wanawauzia hawa wageni maeneo, kinyume na taratibu na sheria.
Wananchi wanahitaji maeneo yao, hivyo wasaidiwe ktk hili.
.......