Uzi Maalumu: Kero, changamoto na suluhu katika sekta ya Kilimo na Mifugo

Uzi Maalumu: Kero, changamoto na suluhu katika sekta ya Kilimo na Mifugo

Messenger RNA

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
1,498
Reaction score
3,881
Ndugu wadau wa Jamii Forum As-salamu alaykum, Bwana Yesu asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Majeshi Majeshi.
Kama mnavyofahamu, viongozi na wadau wengi wenye dhamana ya kufanya maamuzi hupita na kusoma maoni katika jukwaa hili. Ili kuwa na sauti ya pamoja na yenye nguvu, nimeona ni vyema kuanzisha uzi huu maalumu utakaokusanya kero zote zinazowagusa wakulima, wafugaji, wafanyabiashara na watoa huduma.

Lengo kuu ni kuweka changamoto hizi sehemu moja ili wahusika (viongozi na watunga sera) wanapopita jukwaani hapa, wazione kwa urahisi na kuzifanyia kazi.

Uzi huu utajumuisha kero za:
• Uzalishaji: Pembejeo, mbegu za mifugo na mazao, viuatilifu na madawa ya mifugo, na miundombinu;
• Taasisi za Kifedha: Mikopo ya kilimo/mifugo na bima;
• Ushirika: Changamoto za AMCOS na vyama vikuu vya ushirika kwa Sekta ya Kilimo na Mifugo;
• Utolewaji wa huduma za kilimo na mifugo;
• Masoko: Bei ndogo, changamoto za vipimo (lumbesa), na masoko ya uhakika; na
• Masuala mengine yote yanayohusu hizi Sekta mbili.

Karibuni sana tuseme neno, tuchangie kero zetu kwa ustaarabu na kutoa mapendekezo ya suluhu ikiwezekana. Uwanja ni wenu!
 
Back
Top Bottom