Mkuu hii inasaidia vipi kuhusu kuporomoka kwa thamani ya shilingi yetu dhidi ya US dolar na sarafu nyingine za kigeni?
Hili sio jukwaa la Uchumi hili swali ungelipeleka kule usimkatishe tamaa mtoa mada
swala la kuporomoka kwa shillingi yetu sisi sio wa kwanza ziko nchi ambazo hela yao imeporomoka mno dhidi ya dola lakini zina maendeleo makubwa kuliko nchi yetu nitakupa mfano
Nchi ya Indonesia dola yake moja ni sawa na rupia za Indonesia 15,236
Sisi dola moja ni sawa na shillingi 2493
Je kati ya sisi na Indonesia nani wameendelea kama sio wao?
Nchi ya Comoro dola moja ni sawa na faranga 449 ina maana ina dhamani kuliko sisi lakini ajabu kati ya nchi masikini nao wapo tumewazidi mbali mno.
Msumbiji ni masikini kuliko sisi lakini dola moja ni sawa na meticall 63.
Italy ni nchi iliyoendelea mno na viwanda na katika G5 nchi zenye viwanda duniani na maendeleo makubwa lakini sasa ukiambiwa dola moja ni sawa na lira 1,828
Hela yenye thamani kuliko nchi yeyote duniani kuliko hata Marekani yaani dola ya marekani ni kuwait
Dola 100 za marekani ni sawa na dinar 31 tu lakini marekani ndio nchi iliyoendelea kiviwanda na kijeshi kiliko kuwait.
Kuna ka nchi kanaitwa Eritrea ni masikini kuliko Tanzania hela yao inaitwa Nakfa lakini dola moja ni sawa na Nakfa 15
Mambo ya uchumi ni magumu sana kuelewa huwezi kukaa tu kwenye kiti una discuss dola kushuka we kunywa ugimbi wako fanya kazi mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe ya kaisari mpe kaisari ya Augusto mpe Auguto ya mungu mpe mungu.
Haya mambo waachie benki kuu ndio wanajua sisi hapa kijiweni tunaelimishana mambo mengine kabisa