Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Natafuta nyimbo moja walikua wanaimba hivi

" mimi nikijiona nikama sitakufa kumbe najidanganya maisha sio kitu mali zangu zote watachezea wengine"

Nakumbuka tuu hivyo vipande Ila kwaya nime isahau naomba hii nyimbo
Huo wimbo umeimbwa na kwaya kuu Moravian mbeya, unaitwa maisha nisawa na maua
 
Umeuliza kuhusu Sedekia na RHM, ni kwamba Sedekia alishaimba na New Life Band, kama unawajua hawa vijana na band yao.

Ila Tanzania nzima walikuwa wanarekodi RHM.

Sidhani kama itatokea tena Gospel band kama NLB Tanzania

Na sio Sedekia tu ila pia kuna Upendo Kilahiro na Beatrice Muhone.

NLB Walitunga mapambio kama:-

- Iende mbelee injili hiyoo...iende mbeleee

- Ainuliwe Mungu wetu leooo...ainuliwe bwana wa mabwana

- Mji ulee una meremeta umepambwa mauaaa

Unakumbuka?

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
New life band naweza kusema ndio waasisi wa mapambio mengi sana ambayo ndio yanaimbwa hadi hivi leo, sijui lile kundi lilikuja kuwaje au biashara ya magari ya mchanga na shule viliwazidia
 
Hawa wana nyimbo hatari sana,wananukuu maandiko sana alafu wana upako mpaka unaona Mbingu zimeshuka loh!
Kilimanjaro revival kwa askofu Lazaro..? Nimesali hapo miaka mitatu yule baba MUNGU ambariki sana ndiye aliye wapika kina pastor Naomi ambaye alikua rombo labda kama amerudi pale
 
Habarini, naombeni kuungwa kama kuna hilo group la old is gold 0626239563. Natanguliza shukran[emoji120]
 
Nimefuatilia chatting kama yote, kwa kweli binafsi napenda sana nyimbo za kitambo,
 
Wakuu poleni na majukumu…..kuna hii albamu ya kijitonyama choir kabla hawajagawanyika ina nyimbo kama….
1. namtafuta bwana
2. anipenda bwana yesu
3. masia wanyi
4. simba wa yuda
5. shauri yako
6. hakuna mungu kama wewe na
7. bwana ndiye mchungaji wangu
Je naweza pata nyimbo za hii album? kipindi hicho zilikuwa katika mfumo wa kwenye tape….Sina uhakika kama zinapatikana katika mfumo wa kisasa but nazitafuta sana bila mafanikio na bado nina shida nazo sana…...msaada plz
Audio ninazo kasoro original ya Shauri yako, ambayo ndo naitafuta
 
Haha old is gold

Kuna wimbo najitahidi kuukumbuka hapa, unanigomea. Nakumbuka tu sehemu hii kidogo, ni story ya mwanamke Msamaria

"Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia
Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwa Msamaria
Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria"
Hiyo iliimbwa na eben ezer kwaya kutoka pale t.a.g mbagala kizuan kwa makamu askofu mkuu wa t.a.g dr magnus muhiche
 
Back
Top Bottom