Uzi maalumu kwa ajili nyimbo za injili za zamani(Old school Gospel songs) za Tanzania!

Natafuta nyimbo moja walikua wanaimba hivi

" mimi nikijiona nikama sitakufa kumbe najidanganya maisha sio kitu mali zangu zote watachezea wengine"

Nakumbuka tuu hivyo vipande Ila kwaya nime isahau naomba hii nyimbo
Huo wimbo umeimbwa na kwaya kuu Moravian mbeya, unaitwa maisha nisawa na maua
 
New life band naweza kusema ndio waasisi wa mapambio mengi sana ambayo ndio yanaimbwa hadi hivi leo, sijui lile kundi lilikuja kuwaje au biashara ya magari ya mchanga na shule viliwazidia
 
Hawa wana nyimbo hatari sana,wananukuu maandiko sana alafu wana upako mpaka unaona Mbingu zimeshuka loh!
Kilimanjaro revival kwa askofu Lazaro..? Nimesali hapo miaka mitatu yule baba MUNGU ambariki sana ndiye aliye wapika kina pastor Naomi ambaye alikua rombo labda kama amerudi pale
 
Habarini, naombeni kuungwa kama kuna hilo group la old is gold 0626239563. Natanguliza shukran[emoji120]
 
Nimefuatilia chatting kama yote, kwa kweli binafsi napenda sana nyimbo za kitambo,
 
Audio ninazo kasoro original ya Shauri yako, ambayo ndo naitafuta
 
Hiyo iliimbwa na eben ezer kwaya kutoka pale t.a.g mbagala kizuan kwa makamu askofu mkuu wa t.a.g dr magnus muhiche
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…