Uzi maalumu kwa wale waliojifunza kitu baada ya kuhudhuria baadhi ya misiba

Kipenseli

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
825
Reaction score
1,074
Hello! Wana JF natumai mko poa,Husika na kichwa cha habari hapo juu kuwa huu ni zi maalumu kwa wale ambao wametoka sehemu fulani kwa kujifunza kitu kikubwa katika maisha(Hususani misiba).

Zipo faida nyingi sana za kuhudhuria katika misiba ikiwa pamoja na kwenda kufariji wafiwa n.K

*Binafsi yangu nimehudhuria msiba wa mtu ambaye kiukweli simfahamu (Hii ilikuwa baada ya kutoka msikitini swala ya adhuri) na nikaongozana na umati mkubwa uliokuwa umeingia hapo msikitini. Kwa mara ya kwanza nimejikuta nikilia katika msiba (huo) wa mtu ambaye simfahamu na sijawahi kuonana nae ila inavyosemekana ni dogo tu ambae amefariki akiwa form two,vitu kama sifa zake njema ziliosababisha ule umati kuwepo pale,mawaidha ya yule sheikh nimejikuta nikilia na kuhuzunika ndani ya nafsi yangu huku nikijifunza mengi sana kupitia ule msiba.

Hali hii imeshawahi kukukuta? je umewahi kujifunza nini baada ya kuhudhuria msibani? uwe wa ndugu au wa mtu usiyemfahamu
 
Ule msiba wa mtoto wa Muna Love, nimejifunza kuwa kuna wanawake wanatuona sisi wanaume mandondocha, mtoto ana baba wawili na wote amechukua Child support hadi mwisho.
Patrick kama sijakosea
 
Marehemu amefariki kwa malaria na U.T.I ijapokuwa wapo watu wanaishi kwa U.T.I kwa zaidi ya miaka mitano na Mungu ameamua kumchagua yeye
 
Watu wasiokuwaga na imani na masuala ya kidini ukihusisha na roho/nafsi wanapohudhuria kwenye misiba wana reason kitu na kuanza kuzisoma dini....Sio watu wote lakini ni wale wanaoguswa na kujifuNza kitu


Kuna misiba iko very sensitive
 
Ule msiba wa mtoto wa Muna Love, nimejifunza kuwa kuna wanawake wanatuona sisi wanaume mandondocha, mtoto ana baba wawili na wote amechukua Child support hadi mwisho.
Hivi iliishaje ni yule wa mawingu media au huyu baba mwingine ndo aloweza kuchukua nafasi?
 
Mimi nikikosaga msosi huwa naumia sana [emoji16][emoji16][emoji16]

Kufa sote tutakufa tu. Uzikwe na watu milioni au mtu mmoja haikusaidii cho chote. Ila ni muhimu kutenda mema tukiwa bado hai ili tusiwafanye watu kudanganyana wakati wakisoma eulogy zetu. Mungu na Atusaidie [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Basi kuna kitu umejifunza zaid ya hicho ulichosema na nimekuelewa[emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…