Uzi maalumu: Matukio yaliyochukiza kwenye Awamu ya Tano

Uzi maalumu: Matukio yaliyochukiza kwenye Awamu ya Tano

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Huu ni uzi maalumu.

Nakusudia tujikumbushe matukio ambayo sio mazuri na yabaki kuwa kumbukumbu.

Nitataja machache na wengine wataweka yaliyosahaulika.

1. Kupigwa marufuku mikutano ya kisiasa na maandamano isipokuwa mikutano ya ndani na ya wabunge Katika maeneo yao
2. Kuibuka wimbi la kupotea wanasiasa wa upinzani akiwemo Mawazo na Ben Saanane

3. Kutokea wimbi la kuokotwa maiti kwenye viroba na kutopatikana majibu

4. Uvamizi Wa vituo vya polisi sitakishari, kibiti na kufuatiwa na mauaji

5. Kutokea Kwa majambazi huko amboni Tanga.

6. Kufunguliwa Kwa kesi nyingi kwa wapinzani katika muda mfupi.

7. Kutokea uhasama baina ya chama tawala na baadhi ya vyama makini hasa chadema.

8. Dola kujiingiza kwenye mgogoro wa CUF na kuegemea upande mmoja wa mgogoro

9. Hali ya maisha na kipato cha watu kudorora

10. Sekta binafsi kuanguka na wat u kukosa ajira hasa miaka ya awali ya awamu ya tano.

11. Vyombo vya dola kujiingiza kwenye siasa za wazi, Polisi na wakuu Wa mikoa

12. Wafanyakazi kutopandishwamishahara Kwa kipindi chote

13. Watu kutokuwa na furaha na wafanyakazi kuwa na hofu kwenye mazingira ya kazi hasa serikalini

14. Kushuka Kwa kasi mshikamano Wa kitaifa na kuwepo na chuki za kisiasa kuliko kipindi chochote baada ya uhuru.

15. Kushuka Kwa diplomasia yetu na kuibuka Matamko mengi ya kukosowa kutoka kwa wada u Wetu Wa kimataifa.

16. Kutungwa sheria tata za Habari za mtandao na maudhui ambazo zinalalamikwa sana na wadau.

17. Kuminywa kwa uhuru wa habari na kujieleza

NB. Hayo ni baadhi tu, na sio kwamba hakuna mazuri hapana.

Mada hii imejiegemeza kutaja yasiyofurahisha, MTU mwengine anaweza kuanzisha mada ya mazuri.

Unaweza vilevile kuongezea.

Kishada
 
Kiongozi mkuu KUB kulewa na kisha kuanguka kwenye ngazi mpaka kuvunjika mguu.

Hili tukio litafanya niichukie pombe sana.
 
Watu kuponda kila nzuri linalofanywa na rais, hivi binadamu mumeumbwa vipi kwa kweli maana ningekua rais wa nchi mngekoma sana watu, urais ni shughuli, unakesha ukiwaza jinsi gani ya kuboresha maisha ya watu, halafu kuna mijtu kila siku inakesha ikiwaza kuponda kila kitu hamna hata kimoja kizuri, wao kwao kila kitu ni kibaya na hakifai.
 
Wakulima wa Korosho kudhulumiwa korosho zao.

Wanajeshi kubeba korosho na kuanza kuuza magunia ya korosho kwa watu wenye hela kwa bei ya chini (Gunia la laki 3 waliuza kwa laki 1)

Wakulima wa Mbaazi kuambiwa wale tu mbaazi zao kwani zina protini.
 
Watu kuponda kila nzuri linalofanywa na rais, hivi binadamu mumeumbwa vipi kwa kweli maana ningekua rais wa nchi mngekoma sana watu, urais ni shughuli, unakesha ukiwaza jinsi gani ya kuboresha maisha ya watu, halafu kuna mijtu kila siku inakesha ikiwaza kuponda kila kitu hamna hata kimoja kizuri, wao kwao kila kitu ni kibaya na hakifai.
Si aache kama kazi ngumu, kuna Wa-tz milion 59.
 
Lissu kushambuliwa kinyama na hakuna aliyetiwa mbaroni kufuatia hili tukio,wakamnyima matibabu,kuzuia mshahara wake na hatimaye kumfukuza ubunge akiwa katika hatua za mwisho za matibabu yake nje ya nchi.

Badala ya kuwatafuta wahalifu,Polisi na watu mbalimbali wa CCM/ Serikali wanaendelea kumsakama Mh.Lissu na Dereva wake huku wakiwakingia kifua wahalifu waliomshambulia.

Jinsi jambo hili linavyoshughulikiwa ukilitazama kwa jicho Huru utapata picha isiyo nzuri.Pengine Polisi,CCM na serikali yake hawajajipanga kutenda jambo lolote kuisaidia CHADEMA na/au kuwatendea haki.

Tuepuke chuki dhidi ya Watanzania wenzetu.
 
Hoja yako nzuri lakini kwa mtazamo wangu hukupaswa kuanza na mambo ya kisiasa japo uchumi, Jamii hata Afya yote ni matokeo ya siasa. Ungeanza na issues zinazogusa watanzania wote wanasiasa na wasio wanasiasa then ukaja na hizo za maandamano na mauaji. Mfano:
1. Bomoabomaa e.g Dar
2. Unyanyasaji wa dada kaka, mama na baba zetu kwa kusingizio cha vyeti fake!
3. 15% rejesho la mikopo ya elimu ya juu. Hii % ni kubwa zaidi ya benki wakati mkataba ulikuwa 8%
4. Kodi kubwa TRA zisizoendana na ukubwa wa biashara!
 
Kiongozi mkuu KUB kulewa na kisha kuanguka kwenye ngazi mpaka kuvunjika mguu.

Hili tukio litafanya niichukie pombe sana.
Watu kuponda kila nzuri linalofanywa na rais, hivi binadamu mumeumbwa vipi kwa kweli maana ningekua rais wa nchi mngekoma sana watu, urais ni shughuli, unakesha ukiwaza jinsi gani ya kuboresha maisha ya watu, halafu kuna mijtu kila siku inakesha ikiwaza kuponda kila kitu hamna hata kimoja kizuri, wao kwao kila kitu ni kibaya na hakifai.
Yalomchukiza nani? wewe na mumeo?
Michango ya wabunge wa Chadema kuliwa na Mbowe na madem zake
Mbowe kuchakaza papuchi za wabunge wa kike wa CDM, akitumia ruzuku ya chama na nguvu ya nyagi!!
Ukabila, usukuma, ukanda ya ziwa, mambo ya kienyeji, ushamba, chattle kwanza.
 
1. Ukosefu wa ajira, vijana wengi mitaani hawajuwi leo na kesho yao.

2. Kuzuwia bunge live

3. Fukuzafukuza ya wabunge wa upinzani bungeni

4. Wabunge wa chama tawala asilimia kubwa kuwa wazushi, na kutochangia hoja bungeni ila kuponda upinzani.....

5. Bunge kujiunganisha na serikali, hakuna tofauti

6. CAG kunyanyaswa, Prof Assad

7. CCM kufanya mikutano popote nchin wapinzani wakikataliwa

8. Wakuu wa mikoa na wilaya kujiweka ccm 100% nakuwa wapiga debe na wanyanyasaji wa wapinzani, Iringa, Mbeya, Arusha, Hai, dodoma na Dar es salaam

9. Watu kubamkiwa makesi

10. KATIBA KUPUUZWA
 
Hoja yako nzuri lakini kwa mtazamo wangu hukupaswa kuanza na mambo ya kisiasa japo uchumi, Jamii hata Afya yote ni matokeo ya siasa. Ungeanza na issues zinazogusa watanzania wote wanasiasa na wasio wanasiasa then ukaja na hizo za maandamano na mauaji. Mfano:
1. Bomoabomaa e.g Dar
2. Unyanyasaji wa dada kaka, mama na baba zetu kwa kusingizio cha vyeti fake!
3. 15% rejesho la mikopo ya elimu ya juu. Hii % ni kubwa zaidi ya benki wakati mkataba ulikuwa 8%
4. Kodi kubwa TRA zisizoendana na ukubwa wa biashara!
Ushauri umezingatiwa na nyongeza imepokelewa
 
Umasikini kwa watumishi wa umma haijawahi tokea tangia mkoloni
 
viongozi kuwa kama maroboti ya kutekeleza amri kutoka mawinguni
 
Wasanii wa muziki na burudani kutumika kupiga kampeni waziwazi kwa mapambio na shangwe hilo linatokana na kipato kidogo kinachopatikana ktk sekta ya muziki na burudani chini ya usimamizi wa BASATA hivyo wanakuja kwenye siasa ili wajaze mifuko yao kupiti pesa za CCM. HAPA NAYAZUNGUMZIA MATUMIZI MABOVU YA SHOBO
 
Back
Top Bottom