Uzi maalumu: Tukumbushane mazuri ya viongozi wetu

Uzi maalumu: Tukumbushane mazuri ya viongozi wetu

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Uzi huu ni mahususi wa kuyakumbuka mazuri ya viongozi wetu ambao wa ngazi ya kitaifa. Viongozi hawa ni wa kisiasa ambao wapo serikalini au kambi ya upinzani. Viongozi ambao wapo hai au wametangulia mbele za haki.

Niwaombe wanajukwaa tufunguke yale mambo ambayo binafsi yamekugusa. Kama kuwakosoa tunafanya hivyo kila mara na inawezekana mabaya yao yanazidi mazuri yao, lakini hapa tuyaweke mazuri yao yaani upande wao ambao waliwahi kuonesha ubinadamu, utu, usaidizi, wema na lolote chanya.

Tuyakumbuke mema yao pia.
 
Nakumbuka Mama Samia akiwa Makamu wa Rais alienda kumtembelea Tundu Lisu hospitalini Nairobi alipokuwa amelazwa baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi mchana kweupee huko Dodoma.
 
Nakumbuka maneno ya Magufuli akiwa waziri, pale alipowaambia wakazi wa Kigamboni kuwa wapige mbizi tu baharini endapo wangeona kuwa nauli ya kivuko iliyopendekezwa na wizara yake kuwa hawaimudu.
 
Mwaka 2003 alifariki msanii mmoja nguli wa muziki wa asili. Alifia Sweden alipokwenda kwa shughuli binafsi.
Hali olikuwa ngumu kiasi hela ya kusafirisha mwili wake ilipelea baada ya baadhi ya watanzania wanaoishi hukk na wasanii kujichangishana....

Nakumbuka mzee Jakaya Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Wasanii walibisha hodi wizarani na akawapokea, alifanikisha kulipia gharama za kuuleta mwili wa Marehemu Charles Zawose na akazikwa kwao Bagamoyo pembezonu mwa kaburi la mjomba wake Hukwe Zawose kwa heshima.
 
RIEP Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mchonga meno! Maono yako ya Tanzania ya viwanda yalilifanya Taifa kuwa na viwanda vyake lenyewe zaidi ya mia moja, tena vyenye kutoa bidhaa bora na za viwango vya kimataifa
 
Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Uzi huu ni mahususi wa kuyakumbuka mazuri ya viongozi wetu ambao wa ngazi ya kitaifa. Viongozi hawa ni wa kisiasa ambao wapo serikalini au kambi ya upinzani. Viongozi ambao wapo hai au wametangulia mbele za haki.

Niwaombe wanajukwaa tufunguke yale mambo ambayo binafsi yamekugusa. Kama kuwakosoa tunafanya hivyo kila mara na inawezekana mabaya yao yanazidi mazuri yao, lakini hapa tuyaweke mazuri yao yaani upande wao ambao waliwahi kuonesha ubinadamu, utu, usaidizi, wema na lolote chanya.

Tuyakumbuke mema yao pia.
wakati mzee mwinyi yupo madarakani . wakati msafara wake unapita alipishana na watu wanaenda kuzika alisimamisha msafara wake akashuka kwenye gari akaenda kuungana na watu kubeba jeneza
 
Back
Top Bottom