Uzi maalumu wa Co2 laser engraving machine, ushauri, msaada, vipuri, utengenezaji

Uzi maalumu wa Co2 laser engraving machine, ushauri, msaada, vipuri, utengenezaji

h120

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
2,544
Reaction score
3,361
CO2-Laser-Cutter-Machine-for-Wood-Acrylic-Cutting-Flc1390.jpeg
Kwa wale wote wanaomiliki au ku operate machine tajwa hapo juu, basi karibuni sana nimefungua uzi huu mahsusi kabisa kuwakutanisha watumiaji wa machine hizo, lengo ni kukabiliana na changamoto mbalimbali kwenye uendeshaji na utunzaji wa hizo machines.

Kuna baadhi ya watu waliagiza machine hizo wamezitumia kwa muda mfupi zikapata shida mbalimbali na hivyo kushindwa kupata msaada kwani hamna mafundi wengi waliojilita katika ukarabati na pia uhafifu wa upatikanaji wa vipuri.

Nawakaribisha wote tubadilishane mawazo na kusaidiana kwa wale waliokwama, uamuzi wa kufungua uzi huu ni kwamba sijaona page au forum yoyote kwa hapa Tanzania ambayo imejikita kwenye hizo machine basi hii itakua fursa pekee ya kuwaunganisha wamiliki wote wa machine hizo.

NB
Kwa wasiozijua hizo machine mnaweza kutumia mjomba google, mniwie radhi sintoweka utangulizi au utambulishi.

Tutachambua part moja moja kadri uzi utakavyokwenda.
 
Aina za controller zinazotumika.

1. Lihuiyu M2 controller (M2 NANO)
Hii controller inatumika sana kwenye machine nyingi, wanunuzi wengi huanza na machine zenye hizi controller, haina features nyingi, na bei ya hizi controller ni ndogo, zinacheza kati ya 20$-40$
Kama mtu una mpango wa kununua machine mpya epuka kuchagua hizi controller

lihunyu m2.jpeg



2. Ruida controllers
Hizi ni dsp controllers ndio controller bora kabisa kwa sasa kwenye soko, zina bei kubwa, ukichagua machine yenye aina hii ya controller basi na bei ya machine hupaa.

Moja ya sifa ya hii controller ni uwezo wa kuendelea na kazi baada ya umeme kukatika unaweza resume kazi pale ilipoishia, ina sifa nyingi nzuri,

Bei ya hizi controller ni 290$-350$
6442.jpeg


6445.jpeg



Zipo aina nyinginezo pia , ila hizo tajwa ndio maarufu zaidi.

Kama ulinunua machine ina M2 NANO controller unaweza ku upgrade kwenda Ruida ila itakugharimu si chini ya milioni moja kufanya hizo upgrades.
 
Back
Top Bottom