Uzi maalumu wa kuchambua maana ya mashairi ya nyimbo

Uzi maalumu wa kuchambua maana ya mashairi ya nyimbo

zagarinojo

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2020
Posts
2,622
Reaction score
2,846
Muziki ni moja ya burudani kabambe kwa hapa Tanzania inaamsha hisia,kuelimisha na kusisimua.

Hata hivyo wasanii wanatumia lugha za kimafumbo wakati mwingine.

Unaonaje kama tukijaribu kuchambua na kutambua maana ya mashairi hayo hapa!
Itapendeza sana.

Kwa mfano
Wimbo wa Mrisho Mpoto-Salamu Zangu

Mpendwa Mjomba,tumetenganishwa na ukuta,
Sidhani kama utatutembelea tena kama msimu uliopita,
Japo kwa sasa utakuwa adimu pokea salamu zangu,

Ukienda msibani aliyefiwa utamjua atakuwa amevaa tofauti na wenzake na machozi yasiokauka,
Mimi najua ni wewe mfiwa uliye na huzuni msiba wetu kuubeba,

Ala moja haikai panga mbili,
Vimba lisilo akili waswahili husema ni gogo,
Taja magogo yote la mbuyu si la mvule.


Au unaweza kuchagua kasehemu kadogo ka wimbo kwa mfano

Diamond Platnumz-Baila
"Utamu wa big G ni kutafuna usimeze uroda"
 
Sio kwa chanjo za bilgate, ndio mtapona.../
Msije kustuka mkiwa really late, juu ya corona.../
 
Walitaka kumuwinda simba, kumshika wakashindwa.../

Akawa boss wa redio na kituo cha runinga, anavimba.../
 
Young killer
Sinaga Swagga

"kichwani hamna shule,
Demu wako anajiuza halafu na bei
Ni kama bure,
 
Baada ya kuzama naibuka na mada, tega sikio fuatilia simu ya dada.../

Sio mwingine huyu ni dada tele, anasimu kali unaweza piga mpaka mbele.../

Ina shimo moja la kuchomekea chaji, anaijali sana anaitumia kama mtaji.../

Simu yake inafanya apate mabwana, anavyolinga nayo utadhani wengine hawana.../

Wajanja wanaiminya kwa vidole, ilivyo kali mpaka wenzie wanataka wampole.../

Simu ya dada hua haipigwi na maboya, maana ni kali na nje ina kava la manyoya.../

Aliniambia bila simu haishi mjini, haiachi nyumbani mda mwingi inakaa mwilini.../

Ina jicho la camera kali kinoma, fungua bluetooth uone anavyo rusha ngoma.../

Walipiga watu kumi alivyo lewa cham, nilidata simu ya dada hata mimi siifahamu.../
 
Hii siyo picha ya kihindi, katikati hakuna nyimbo.../
Hii ni zaidi ya movie, achana na isidingo.../

Kubwa la maadui hasikilizi wenzake, anafanya anachofikiri kwenye akili yake.../

Ameshindwa van damme ameshindwa jet li, sijui star gani atashinda movie hii.../

Hii movie hata trela sio bure, wanakufa mastar ila jambazi ni yule yule.../

Adui mwenye nguvu, ukimtazama kichwa chake aisee unaweza ukadhani fuvu.../

Akipita barabarani gari zote pembeni, na usijaribu kusema ye ndiye chanzo cha foleni.../

Ngoja nione itaisha vipi movie ya leo, ikiisha bila maandishi mi nitavunja video.../

Sio siri, jambazi kuu amezidi ukatili.../
Na anajiandaa mwakani aigize movie ya pili.../
 
Back
Top Bottom