zagarinojo
JF-Expert Member
- Jul 26, 2020
- 2,622
- 2,846
Muziki ni moja ya burudani kabambe kwa hapa Tanzania inaamsha hisia,kuelimisha na kusisimua.
Hata hivyo wasanii wanatumia lugha za kimafumbo wakati mwingine.
Unaonaje kama tukijaribu kuchambua na kutambua maana ya mashairi hayo hapa!
Itapendeza sana.
Kwa mfano
Wimbo wa Mrisho Mpoto-Salamu Zangu
Mpendwa Mjomba,tumetenganishwa na ukuta,
Sidhani kama utatutembelea tena kama msimu uliopita,
Japo kwa sasa utakuwa adimu pokea salamu zangu,
Ukienda msibani aliyefiwa utamjua atakuwa amevaa tofauti na wenzake na machozi yasiokauka,
Mimi najua ni wewe mfiwa uliye na huzuni msiba wetu kuubeba,
Ala moja haikai panga mbili,
Vimba lisilo akili waswahili husema ni gogo,
Taja magogo yote la mbuyu si la mvule.
Au unaweza kuchagua kasehemu kadogo ka wimbo kwa mfano
Diamond Platnumz-Baila
"Utamu wa big G ni kutafuna usimeze uroda"