Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

majoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2013
Posts
2,595
Reaction score
4,775
Wakati mwingine katika maisha tunapitia vipindi vigumu na vizito vinavyotufanya tuhitaji kufarijika na kutiana moyo. Unaweza kufarijika kwa maneno mazuri toka kwenye vitabu vya dini au toka kwenye mawazo ya mioyo ya wengine. Sio vibaya tukawa tunatiana moyo humu na kufarijiana.

Jaribu kuandika kitakachoweza kufariji au kutia moyo ili kila atakayepita hapa afarijike.

Hasa katika kipindi hiki hali tunayopitia, maisha magumu, kazi hatuna, mafisadi wanakula jasho letu .... tunapambana tu... lazima tugangamale

Zaburi 46 inasema.

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Bwana wa majeshi yupo pamoja nasi.
 
N
maisha hayako kama tulivyokuwa tunaambiwa lakini jambo la uhakika kifo kipo mbele yetu

Na hatutakiwi kuogopa kifo maana ndio njia ya kwenda hukooooooooo. Kifo ni lazima so Usiogope Ujapopita katika bonde la uvuli wa mauti, Mungu hatakuacha atakuwa pamoja na wewe. Jiandae kufa.
 
Isaya 41
6. Wakasaidiana kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake uwe na moyo mkuu

Jamani tusaidianeee hata kuchangiana pesa za kusomesha watoto/ndugu zetu. Kipindi tunachoishi ni sheeeedah
 
7. Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike.

Tutiane moyoooooo
 
Back
Top Bottom