Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Duuh maisha haya aah sijui ni bongo tuu adi unajihurumia
 
Mkuu umegusa hadi matatizo yangu ha ha ha ha

Kila siku lazim nickilize wimbo wa prof ft harmonize-yataisha
 
Pole mkuu. Ukipata muda share
 
Wale wenye shida ya hela ya haraka pia tunahitaji faraja? Kama ndio naomba na mimi mnifariji.
 
Kukata tamaa ni umaskini ukatae.
Kabla hujataka kufarijiwa jiulize ni wangapi wanahitaji faraja yako hali wewe umekata tamaa.?
Nilishawahi kukata tamaa nilivyokua mjamzito. Kama kujiua isingekua dhambi ningeshapotea kwenye ulimwengu huu. Mama yangu nae alikua sababu ya mimi kutojiua. Miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito nilipata tabu sana. Machozi kila siku. Kila nikiamka nawaza kutoa ujauzito au nizae niwe single mom dunia ije kunihukumu. Lakini Mungu ni mwema sana. Nilisema kama ambavyo napata mawazo ya kuwa mama wa huyu kiumbe basi na Mungu hatoniacha.
Sasa hivi hata nipitie gumu kiasi gani hata kulia nimeacha nikiwaza kuna binadamu anaishi kwa sababu mimi nilimleta duniani.
Ninachomaanisha hata upite magumu kiasi gani kuna watu bado wanaamini katika wewe hivyo usikate tamaa. Chukulia kama kipindi cha mpito yote yatarudi kama mwanzo mapito yako yakiisha.
 
Kila mtu anapitia magumu yake

Saiz nipo kweny mwendokas la kutoka kimara to kivukoni na tumejaa pomoni kweny gari na wote nahis tunaenda kazin ila ukiuliza mishahara utakuta wetu ni chini ya laki tatu na apo una kadigirii kichwan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…