Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Uzi maalumu wa kufarijiana kwa wale wote wanaopita kwenye hali ngumu za kimaisha

Mi niko tofauti kidogo...nawashukuru wale wooote walokuwa na mimi katika kipindi chote cha anguko langu. Kipindi nilichohisi nikwambie peke yangu katika dunia. Lakini kubwa zaidi namshukuru Mungu maana katika kipindi kile ambacho mara nyingi watu ndo hupoteza imani...ila kwangu ilikuwa tofauti. Nilikua kiimani. Hakika nawaambieni Mungu pekee ndo suluhisho. Mungu yupo na anatusikia tukiomba. Kuna wakati hauitaji kulia na kulalamika kwa Mungu, we mwambie matatizo yako na muache akutatulie kwa kadri atakavyotaka. Nilichojifunza katika mapito yangu yote ni kutoa shukrani kwa kila ninalopitia. Maana unaweza jihisi una matatizo ila una afya uko imara. Vipi unawafikiriaje walo mahospitalini?? Mwambie Mungu ahsante na ni salama moyoni mwako kwani una imani na hilo litapita.
 
Mwezi wa 9&10 ni miezi iliyokua migumu kwangu..yani kuna muda nikawa najiuliza au nimekua invisible!! Nilikua ni mtu wa kujifungia tu ndani na kujiuliza maswali mengi mno..kuna muda nilitamani nikilala nisiamke.

Ila nikasema siwezi kujikatia tamaa namna hii...nashukuru sasa angalau nipo vizuri
Namshukuru Mungu kwa nilivyo sasa
 
Ameen
 
Pole wote mnaouguliwa, poleni wote mliofilisika komaeni ipo siku mtainuka tu,
poleni mliodanganywa kimapenzi kisha mkaachwa poleni ila mjikaze mtapata wenzi wengine walio wema kwenu,

poleni wote ambao mabosi wenu wanawanyanyapaa kazini jipeni moyo na kujipanga jinsi ya kupata mtaji wa kujiajiri,

poleni wahitimu wote ambao kwa muda mrefu hamna ajira au mmepata ajira ambayo kipato chake ni kidogo sana kiasi kwamba ukipata pa kutokea utakimbia bila kugeuka nyuma.

Poleni mliofiwa,
poleni mliotumbuliwa siku si nyingi mtapata kazi nyingine.

Poleni sana.
Shukran...
 
Huku Ushirombo hatunaga familia za kishua mkuu, hasa sisi wenye tunaishi kwa shemeji zetu ndio kulala wa mwisho na kuamka wakwanza
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Acha bana
 
Back
Top Bottom