HS CODE
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 1,784
- 4,376
Nimegundua Jf hata ukianza mada kwa kusalimia, wajumbe hawajibu, bali wanaenda moja kwa moja kwenye kuchangia, hivyo kwa leo, sitosalimia.
Kwa wengi hali ni ngumu, iwe walioajiriwa au walioko mitaani, hata hivyo hata wenye unafuu wa maisha, haimaanishi wamesha maliza utafutaji wa pesa.
Inawezekana kwa sasa unayopesa mkononi, lakini hujui ni biashara gani ufanye, au kuna mchongo unausikilizia lakini hujui ukitiki pesa utakayopata uifanyie nini, kubwa kuliko yote kuna watu humu wana mawazo ya biashara lakini wanakosa watu makini wakushirikiana nao.
Uzi huu ni wa kupeana mawazo ya biashara zinazoweza kufanyika bila kujali zinahitaji mtaji wa kiasi gani, hata kama sisi bado hatujaanza kuzifanya au tulifanya zikafeli lakini tunaona upo uwezekano wa watu kuingiza njuruku. Inawezekana pia tukautumia kutafuta watu wanaovutiwa na mawazo yetu na wako tayari kushirikiana kwenye safari ya mafanikio. Mimi naanza na mawazo yafuatayo:
Wazo la kwanza
Kuna wale wenzangu wamesoma masomo ya sayansi, na tunajua kabisa masomo ya sayansi kuna changamoto kwenye practicals kwanini msomi asifungue center kwa ajili ya practicals tu, Ili madogo wasaidike, huku anaingiza pesa. Najua vile vifaa ni gharama lakini kila penye nia pana njia.
Wazo la pili
Zanzibar ni kisiwa chenye mahitaji mengi kutoka nje ya nchi, lakini vingi vinavyohitajika bara vinapatikana kwa wingi. Kuanzia bidhaa za shambani kama, mazao ya nafaka, mifugo mpaka za viwandani. Kwanini tusubiri mpaka waagize nchi za mbali?
Wazo la tatu
Watu wanazaa sana, na kutokana na changamoto za utafutaji wanakosa muda wakuwalea Watoto wao, kwanini msomi usiwaze namna ya kutatua changamoto hii, kwa kuanzisha daycare, unatafuta mdada ambaye utamlipa kulingana na unachopata Ili awatunze watoto na wewe unapata mia mbili mia tatu kuliko kuzurura na bahasha na umecharara?
Hebu ongezea na wewe.
Asante.
NB: Nimepata inspiresheni ya kuandika uzi huu, kutokana na michango ya mwanachama griti thinka Daudi1, kama utasaidia kutatua changamoto za watu, sifa zote apewe yeye. Ukisababisha changamoto lawama zote nipeni mimi.
Moderator, naomba msiuhamishe jukwaa huu uzi, ubaki hapa hapa.