Uzi maalumu wa kuwaombea washkaji zetu waliotutoka enzi za utoto

Uzi maalumu wa kuwaombea washkaji zetu waliotutoka enzi za utoto

osmaney

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2017
Posts
1,042
Reaction score
998
Habari wanaJF

Polen na majukumu piaa hongereni kwa utaftaji. MUNGU awajalie katika utaftaji wenu.

Lengo la huu uzi sio ni kuwakumbuka na kuwaombea washkaji zetu waliotutoka enzi za utoto wetu

Natumani huenda wangekuepo bado wangekua washikaji zetu na tungeshirikiana nao mambo mbalimbali, lakini ndio hivyo kazi ya MUNGU haina makosa.

Naomba tuchukue hii nafasi kuwakumbuka na kuwaombea.

Mbele yetu, nyuma yao😪

Kwa kuanza na Mimi. R.I.P kwa washikaji zangu wote waliotangulia mbele ya haki🙏
 
Neema - scul mate alikufa kwa homa ya kichwa ghafla.

Happy - scul mate alifia mtoni wakati akiwa anaogelea na kuzama.

Mohammed - class mate alikufa kwa kuangukiwa na mti.

Steven - scul mate alipotea ktk mazingira ya kutatanisha na hajawahi kuonekan hadi leo.

Raha ya milele uwape eeeh bwana, na mwanga wa milele uwaangazie, wapendwa hawa wastarehe kwa amani. AMEEEEN
 
Anna- school mate wa std 7, nayakumbuka macho yako makubwa ya duara, ulikua mpole na siku zote ulipenda kuniwekea mkono wako begani mwangu iwe tumekaa au tunatembea, ulikua na ndoto ya kua daktari, Homa ya Mapafu ikakatisha ndoto zako, R.I.P Angel.

Aminu- school mate olevel, ulikua mjanja sana, uliipenda biashara na ulisema utakuja kua mfanyabiashara mashuhuri, nakumbuka tulipokua tunajadiliana mambo makubwa kuliko umri wetu, i'm glad i met you, Malaria ikakatisha ndoto zako, Innalillah wainna illah Rajiun.

Issa- Childhood friend, ulinipenda sana, ulisema ungekuja kunioa no matter what, nilikua nachukia ukianza hizo mada, kila mtu mtaani alijua Issa anampenda Culture, tulikua wazee wa kamati kwenye mambo yote yaliyohusu shughuli za watoto na vijana, ulipenda sana muziki na kudance, barabara ile ya Victoria ikakatisha uhai wako, Rest Easy Mwamba.

Deo- daah ukanipigia simu unataka kurudi kwenu ukasalimie wazazi wako, kumbe ndio uliniaga jumla, yale maji ya bahari yakaondoka na roho yako, R.I.P Besty, ulikua huongei lakini ukiwa na mimi unapiga story tunacheka, walikushangaa hadi wakakuzoea. [emoji24]
 
2012 mshkaj wng straton baada ya furaha ya sisi kumaliza olevel siku ya graduation ulikuwa na pikipiki furaha zilizidi kumbe ile siku ndio ulikuwa mwisho wako uliniambia unachomoka mara moja unaenda road apo kufuata fegi baada ya dk5 nasikia ukunga uku watu wakikimbilia barabarani kumbe ukiingia na pikipiki chini ya semi kichwa kikafumuka na ndoto zako zikaishia hapo hapo nakujuza tuu ulipo baada ya wewe kuondoka matokeo yalikuja umepata Div2 nalikumbuka sana shati lako jeupe jipya ulilovaa ile siku ila ghafla lilikuwa jekundu. Nakukumbaga Sana mpaka leo na nakuombea uendelee kupumzika kwa amani. Amen
 
Dua Said, my classmate Mahiwa Sec. Alilazimika kukatwa mguu baada ya kansa kumshambulia, bado haikufaa kwa yeye kuendelea kuishi duniani hatimaye akafariki miezi kadhaa mbele. Bado nakukumbuka sana Mahiwa Boy.

Abby, friend wa ukubwani. Baada ya miaka mingi ya kutoanana nikapokea tarifa ya kifo chako. Ilikuwa ngumu kupokea lakini hakukuwa na namna. R.I.P Swahiba, Nyangao inakumiss.
 
Neema - scul mate alikufa kwa homa ya kichwa ghafla.

Happy - scul mate alifia mtoni wakati akiwa anaogelea na kuzama.

Mohammed - class mate alikufa kwa kuangukiwa na mti.

Steven - scul mate alipotea ktk mazingira ya kutatanisha na hajawahi kuonekan hadi leo.

Raha ya milele uwape eeeh bwana, na mwanga wa milele uwaangazie, wapendwa hawa wastarehe kwa amani. AMEEEEN
R. I.P kwa wote apoo
 
Back
Top Bottom