Anna- school mate wa std 7, nayakumbuka macho yako makubwa ya duara, ulikua mpole na siku zote ulipenda kuniwekea mkono wako begani mwangu iwe tumekaa au tunatembea, ulikua na ndoto ya kua daktari, Homa ya Mapafu ikakatisha ndoto zako, R.I.P Angel.
Aminu- school mate olevel, ulikua mjanja sana, uliipenda biashara na ulisema utakuja kua mfanyabiashara mashuhuri, nakumbuka tulipokua tunajadiliana mambo makubwa kuliko umri wetu, i'm glad i met you, Malaria ikakatisha ndoto zako, Innalillah wainna illah Rajiun.
Issa- Childhood friend, ulinipenda sana, ulisema ungekuja kunioa no matter what, nilikua nachukia ukianza hizo mada, kila mtu mtaani alijua Issa anampenda Culture, tulikua wazee wa kamati kwenye mambo yote yaliyohusu shughuli za watoto na vijana, ulipenda sana muziki na kudance, barabara ile ya Victoria ikakatisha uhai wako, Rest Easy Mwamba.
Deo- daah ukanipigia simu unataka kurudi kwenu ukasalimie wazazi wako, kumbe ndio uliniaga jumla, yale maji ya bahari yakaondoka na roho yako, R.I.P Besty, ulikua huongei lakini ukiwa na mimi unapiga story tunacheka, walikushangaa hadi wakakuzoea. [emoji24]