Uzi maalumu wa kuwaombea washkaji zetu waliotutoka enzi za utoto

wapumzike kwa aman wenzetu, tusichoke kuwaombea🙏
 
usichoke kumuombea mkuu, apumzke kwa aman uko alpo🙏
 
tusichoke kuwaombea wenzetu🙏
 
Mohamed daa ulikuwa mwanangu nakumbuka mwaka 2005 kuna mjinga mmoja alikuzingua ilikuwa pasaka uka mpa kichapo bahati mbaya alikujerui kwa jiwe tuka kupeleka hospitali ya mkoa tulikuwa na mzee Six tulirudi home usiku mkubwaa ukiwa umeshonwa nyuzi nane!

Shaban Mrutu aka Piko ulikatizwa uhai wako kwa ajali ya kugongwa na gari ukiwa na pikipiki ilikuwa Makambako

Jafet Rutahiwa mzee wa vancuva niliskia ulikutwa umefia geto huko Arusha!

Romana kambona daa namis ile mi utani yako!!
NYUMA YENU MBELE YETU
 
Mwanangu wa dhahabu.....UG,eliasi maugo,Arusha sanawari,nakumiss sana mchizi wangu....nakumbuka nilikua dar napigiwa simu kichaa wako wamempiga shokaa,akaangukia mto sanawari.akafa. Christopha aka krisp bado nakukumbuka mwanagu
 
R.I.P khassim
Your browser is not able to display this video.
 
Dah! Uzi wako umenipa kumbukumbu mbili za utotoni hadi leo hazijawahi nitoka kichwani.

Ya kwanza ni primary school. Tulikuwa na michezo ya kuruka sarakasi kwenye milima ya pumba kwenye mashine za kusaga nafaka. Boniface aliruka kwenye rundo moja kumbe lilikua na moto. Hatukua tukijua kuwa pumba huwa tabia ya kuungua kuanzia chini na juu huonekana ziko kawaida. Siku mbili baadae Bony alifia hospital. Taswira yake akiwa ameungua hadi leo haijawahi nitoka kwenye fikra.

'Msiba' wa pili ni primary school pia. Rafiki yetu mmoja, masoud, alipotea tukiwa tunacheza mpira. Wenzetu wa mwisho kumuona walidai alipanda lori la mzee mmoja diwani. Hadi kesho hakuwahi onekana. Tetesi ni kuwa mzee yule alikuwa na michezo ya kutoa kafara. Pumzika kwa amani Masoud.
 
Akida jumbe akida mungu akulinde ulitutoka ghafla ndugu yangu,ndugu zako wa damu bado tupo na cc tunasubiri hatma yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…