Uzi maalumu wa Mfungo Mtukufu wa Ramadhan

Uzi maalumu wa Mfungo Mtukufu wa Ramadhan

Mashaallah, Allah katujalia kuiona ramadhani ingine, tujitahidi kuchangia huu uzi wetu . faizafoxy sijui kaenda wapi jamani?

Ukhuty karibu
 
Nawatakia mfungo mwema mfanye Toba,maana mfungo unaambata na kuswali,nawatakia kila La kheri,kipindi hiki mkitumie vizuri kusikiliza mawaidha na kutenda yaliyo mema,yanayo mpendeza Allah.
 
Nawatakia waislam wote duniani, maandalizi mema ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
 
Assalaam Alaykum Warahmatullah

Tunapenda kunasihiana baina yetu sisi Waislam
Katika kuukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhaan,kuna baadhi huwa na maneno fulani fulani na vitendo viovu
Mfano
VUNJA JUNGU
ni neno linalotumika,kwa wale ambao ni waovu hususan jambo la ZINAA na mfano wake

Hakuna kheri kwako,ikiwa utashikamana na njia chafu katika kuukaribisha Mwezi huu wa Ramadhaan

Hakuna kheri

Kadhalika
Jambo la IBADA YA SWALA
Swala ni moja ya Nguzo Mama kwa kila Muislam Mwanaume au Mwanamke
Mwenye kuacha Sala,Uislam wake upo matatani
Na hakuna Ibada yoyote itakayokubaliwa mbele ya Allah,ikiwa mtu yupo mbali na IBADA YA SWALA
Hakuna Funga,kwa mtu asie swali
Swala kwanza,kisha Funga inafuata
Tusiifanye Dini yetu kimazoea
Dini ina sheria na kanuni zake
Tuwe makini sana,tusiwe ni wenye kushinda njaa,tukidhani tunapata Thawabu,kumbe ni sawa na vumbi au povu
 
Back
Top Bottom