Baada ya wadau wengi kuendelea kufuatilia kwa kuniuliza maswali mengi na kutaka kufahamu juu ya mmea huu na maajabu yake katika tiba ya magonjwa mbalimbali kwa kadri wanavyousikia,leo niandike japo kidogo tu angalau ABC juu ya mtishamba huu.
Mlundalunda ni jina maarufu la mmea huu kwa watu wanaoongea lugha ya asili ya kisukuma,kwa maana ya mikoa ya Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Tabora n.k. Wamasai huuita ORBUKOI.
Zipo species nyingi za mmea huu,aina ninayoizungumzia hapa na ambayo inatumika sana kwenye tiba ni ile ambayo kisayansi inaitwa CASSIA ABREVIATA.Mmea huu unapatikana zaidi katika mapori ya Tabora,pwani na sehemu za umasaini.
Kwa mjibu wa tafiti zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika mpaka sasa,mmea huu ni mzuri sana katika tiba ya magonjwa mengi kwenye mwili wa binadamu,kama utavunwa kwa mazingira sahihi na kuandaliwa kama inavyotakiwa bila kuathiri mlinganyo wake wa kemikali asilia.Mmea huu hutibu mambo yafuatayo;
1. Matatizo ya hedhi na uzazi kwa wanawake, Hususani wanawake waliotharika sana na kemikali za uzazi wa mpango,dawa hii huwarejesha katika hali ya msawazo wa kihomoni.
2. Maralia Sugu; kuna watu wanasumbuliwa na maralia sugu,mmea huu huchanganywa na tangawizi na unatibu changamoto hiyo kwa siku saba tu.
3. Magonjwa ya ngozi,mmea huu unatibu magonjwa aina mbalimbali ya ngozi,hata kama ni mzio wa kuwashwa kila wakati hupona kabisa kwa dosi ya mmea huu
4. Husafisha damu, kama unaenda kupima na unaambiwa damu yako ni chafu ndiyo maana unapata vipele,majipu na kuwashwa mwili,mmea huu hukomesha kabisa hali hiyo kwa kuifanya damu kuwa safi.
5. Huimarisha misuli ya uume, kwa wale wanaume ambao misuli yao ya uume inaonyesha unyonge na wakati mwingine uume unakuwa unarudi ndani ya mwili kama unajificha,mmea huu huondoa kabisa tatizo hilo,kwani ni kiboko ya chango la kiumu ambalo huchangia kusababisha hali hiyo.
6.Hutibu magonjwa ya ngiri.Mmea huu hupambana na chango linalosababisha ngiri kwa wanaume.
7.Kwa kuchanganywa na aina nyingine ya mimea,mmea huu hutibu magonjwa ya PID na kuondoa vimbe katika uzazi kwa wanawake.
Mmea huu unaweza kutumika pekee au kwa kuchanganywa na mmea mingine ili kuleta ufanisi zaidi kwa kuzingatia uwiano maalum kitaalamu.
Unaweza kutumia mmea huu kwa kuchimba mzizi wake mbichi na kuuchemsha,halafu utatumia kwa kunywa mara tatu kwa siku,au kwa unga wa mizizi yake ulioandaliwa kwa ufanisi,nusu kijiko katika maji moto mara tatu kwa siku.
NOTE: Zingatia matumizi sahihi ya dawa kwa kupata ushauri kwa wataalam,jihadhari na matumizi yasiyo sahihi ya mitishamba na hakikisha unatibu tatizo unalolifahamu vyema.
Wasalaam...!
Sent using
Jamii Forums mobile app