Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Dua bora siku ya Arafah ni muhimu kukithirisha kutaja tamko hili , pamoja na dua nyingine na kujiombea mwenyewe ,watu wa karibu ,wa mbali na imma kwa ujumla.
 
Kwa mapungufu tulionayo mtu asipokuwa anapuuzia makosa ya wengine na kufanya kama makubwa amani itakosekana kea kiasi kikubwa.
 
Maneno mazuri sana haya ,Total infatuation upendo huo unaweza kusababisha hata mtu kumuasi Allah kwa kumriridhisha kiumbe na madhara mengine ya kisaikolojia pale anapogundua jambo la utofauti kinyume na matarajio nk

Na hasira sio dhambi kuwa nazo ila mtu asipozicontrol hupelekea maafa makubwa sana kiasi cha kujutia baadae zitakapo poa ,wakati wa hasira Shetani hutumia upenyo huo vizuri kutuchochea majambo ambayo hata hatukuwahi kuwaza kufanya .

Muhimu katika kila hali tuwe Kati na Kati bila kuvuka mipaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…