Alhamdulillah khatimae tumeidiriki ramadhani msimu wa ibada na twaa
ALLAH AWABAARIK NYOTE KWA KUUPATA MWEZI HUU WENYE BARAKA TELE
ikiwa katika mji kuna msimu wa biashara au mavuno basi watu husika wa msimu huo huusubiri kwa mipango madhubuti na imara na kila muhisika atakae zembea kusimamia mipango yake kuonekana hana mana wala umakini na hayupo sawa kwani huenda msimu ujao asiudiriki
kwetu sisi ni zaidi ya msimu tupo katika nyakati za kutafuta radhi na msamaha wa mola mlezi ni jukumu la kila mmoja wetu kusimamia dhamira zake na athibiti katika mipango yake
UMEUANZA VIPI MSIMU HUU WA TWAA NA IBADA ?
Katika kutafuta ujira wa kumaliza quraan mara nne ndani ya mwezi huu ukiwa ndio mpango wetu leo tumesoma juzuu 4 je umeifikia dhamira hii
kwa wale ambao hawana uwezo wa kusoma quraan yote soma kiasi unachoweza kusoma pamoja na kurejea rejea hicho hicho kidogo kwa nia ya kusoma juzuu 4 kwa siku
Niwatakie mwezi wenye baraka kwenu na familia zenu na muwe na swaumu njema yenye uchangamfu wa ibada namuomba Allah atujaalie ikhlaswi katika juhudi zetu na atukubalie juhudi zetu chache tuzifanyazo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.