Tumesoma boarding Boys tupu,nimeingia form 1 shule na suruali tatu na mashati yangu ya tomato matatu yanawaka hatari.
watu walikua wezi ile shule ukianika shati ukigeuka hv kwenda kuchota maji ukirudi kama sio umebadilishiwa shati umewekewa lililo gina basi wameli iba lako kabisa.
nilijitahid kulinda nguo zangu ila wapi ziliibwa moja moja hadi nikabaki na 1 pair yani shati 1 suruali 1, tranka langu nalo wakapita nalo nikabaki mimi na madaftari yangu maana madaftari huwa siweki kwenye tranka
kitandani kwangu ndio library,tranka lilivyoibwa na nguo nlonayo ni 1 pair,nilikua SIjali wala sina habari na mtu nilikua nikitoka darasani nafua nguo zangu naanika nabaki UCHI yani plain natembea hivyo hivyo kila mahali.
waliniita MSANDAWEEEE (bushman) sikua nikivaa nguo kila ninapoenda naenda bila nguo siajli mtu.
Shati langu lililobaki nililikata kuanzia tumboni kuja chini nililikata lote siku za darasani navaa sweta ticha hajui shati langu lipo nusu.
Suruali yangu nikaitoboa matakoni kisha nikashonea kiraka makusudi kama Alama,nguo zangu zilibaki salama salmini na ndio ukawa mtindo wangu hadi sakata langu la kuibiwa nguo HEAD MASTER alipoingilia kati na kusema ole wa mtu aibe nguo zangu. Hapo ndio nikaanza kuwa smart.
ila form 2 na 3 yote nilikua naishi kama msandaweee,u smart nimeuanza form 4 baada ya jina kuwa kubwa shule nzima hamna asiemjua msandaweee hamna asiejua shati la msandawee likoje na suruali zake ule STAR ndio ulipelekea headmaster kunijua na kuniita ofisini kuniuliza KULIKONI.