Mish Albert
JF-Expert Member
- Dec 25, 2015
- 657
- 581
Khabari wanajamvi!!!!
Kama kichwa cha habari kinavyonong'oneza hapo juu
Tunga kisa kifupi cha kutisha kisichozidi maneno 50
Kwa mfano;
1."Ni usiku,upo chumbani kwako unajiandaa kulala
Unasikia sauti ya mama yako jikoni ikikuita
Unatoka chumbani na kuelekea jikoni,ukiwa njiani Ghafla unavutwa mkono kwa nguvu na kurudishwa chumbani
Kuangalia aliyekuvuta ni mama yako,Anakwambia Huku akitetemeka "Usiende mwanangu,hata mimi hiyo sauti nimeisikia"
2.Leo
Ni usiku wa manane,nipo usingizini ghafla mke wangu ananiamsha
Huku mapigo ya moyo wakimwenda mbio
Ananambia,"Mme wangu amka,kuna mvamizi nyumbani"
....Cha ajabu,Mke wangu aliuwawa miaka minne iliyopita na mtu asiyejulikana
3.Kicheko cha mtoto,hufurahisha pale unapokuwa mezani ukila chakula cha mchana na familia yako
Ila huwa tofauti,unapokisikia saa saba za usiku ndani ya chumba chako wakati upo peke yako chumbani
Kazi kwenu!