Wanasuburi kujiachia wakati sipo, Flow zinajiachia bila ushuru hazikatwi kwa max malipo
Tizama na naleta ukafiri,
kwa yangu mistari
nnayochora bila hata ya kufikiri na sikustiri
Kuwa makini yoh babu, kichwani sipo dry na si gongi ulabu
Kwa hii time nnayoandika
Na ujumbe kwako utafika, sina haja ya ku' edit vina kwangu ni kama stika
Na vimeganda
Rest in hell kwa unaye ni diss
Nakutafuna hadi mifupa nna roho kama ya fisi,
Umevuka border unataka shari stimu zangu like thisss
Kaa mbali nami bwana mdogo,
harakati zangu siku nne hukati gogo,
mi ndo doctor njoo nikutibu dogo usijetoa ndogo,
Mabasha kila kona hold on punguza mikogo,
Ukiendekeza utakula mihogo na utakalia vigogo
Ukweli unawatia homa
Nikitema cheche hawaniskizi
wanajifanya wana usingizi unaokoroma
Hawakujua kwamba mimi ndo yule mteule Kuntu
Hii window haichafuki niite iMAC au Ubuntu
Wanasema nipute mchanga kitambo nilishathubutu
Usipoielewa
Sizi, varangati lake kubwa kama umekabwa na jinamizi
So plizi
Mamluki wanan'diss kwa swagga za weezy, Hii ni round two
Kwenye hii game huwa nachelewa kupizi