Uzi wa kijobless

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
UZI WA KIJOBLESS ( c&p:x)

Leo ngoja niwape stori moja hivi.
Kuna siku bhana mteja alinicheki akasema anahitaji mataulo matano meupe. Nikasema haina shida umepata, nipe location akanitajia ila akasema hela ya delivery kubwa sana hadi alipo nikamwambia usikonde kama utaweza vumilia hadi jioni nikiwa natoka.

Nikuletee utachangia hela ya daladala tu kwenda na kurudi, akasema poa. Basi jioni ilivyofika nikamfungia mzigo nikaanza safari mdogo mdogo huku tukipeana maelekezo ya sehemu husika, basi nikafika kweli getini nilipoelekezwa nikaona maandishi yanasoma wanafanya huduma ya masaji.

Nikaona leo humu ndani kutakuwa na pisi za maana si unajua tena basi nikajiweka vizuri kabla sijaingia ndani manake huwezi jua bhana si mnaelewa wanangu hapo eeh, basi nikazama hadi ndani kwa mteja wangu. Nafika tu mapokezi nakutana na dada kavaa kimini na tisheti.

Kifuani chuchu zinachoma nikaona huu ndo ugonjwa wangu kabisa, nikamsalimia nikamwambia kuna dada kaniagiza hizi taulo kasema nimngojee hapa anakuja, akaniambia kaa hapo kwenye kitu kaka yangu mzuri mzuri usijali anatoka sasa hivi yupo na mteja, nikasema sawa ila sasa.......

Alivyoniitaka kaka mzuri mzuri na sauti kanilegezea akanimaliza kabisa na ukiangalia ana sifa zote nazozitaka basi dah nikawa situlii pale kwenye kitu πŸ˜‚. Sijaka sawa akapita dada mwingine kavaa kimini na shati tu vifungo kafungua hadi maziwa yanakalibia kuonekana dah

Nikasema leo kazi ninayo sijatulia vizuri yule dada wa mapokezi akaanza kunichombeza eti "kaka kwani wewe hufanyagi masaji" kwa uchu wa yule dada nilitaka nilopoke nafanya ila nikajizuia nikasema nisipokuwa makini hapa naacha hela ya mataulo hapa hapa ngoja nikaze.

Na mie nikaamua kumzingua hivi kwani mnafanya bei gani akajibu sogea hapa nikuelekeza bei na huduma zetu zilivyo nikaona yes hii fursa sasa ya kumuangalia vizuri huyu mrembo. Kweli nikasogea hadi pale akawa kainama kidogo anatoa karatasi basi kisketi kikapanda kiaina hivi.

Asee akazidi kunichanganya, akaninuka akawa ananionyesha huduma zao mie nikawa nimepatwa wazimu sasa macho yapo kifuani tu kwenye zile chuchu dede sielewi anachoniuliza, bahati nzuri yule dada aliye niagiza matauli akaja ndo akanishtua ikabidi nimwambie nakuja ili anielekeze tena

Basi yule dada alitoka akiwa na upande wa kanga kajifunga tu nali zigo la kwenda asee dah ananiongelesha na sauti ya kimahaba nikaona hapa leo nimepatikana naweza nisitokea salama humu. Basi akakagua mzigo akalizika akanilipa akaniambia save namba yangu nitakuwa nakuagiza vitu

Nikasema poa asante sana ila ngoja nirudi pale mapokezi yuke dada alikuwa ananipa maelekezo ya huduma zenu, nikashangaa anatabasamu alafu ananiambia shauri yako usije ukaacha hela za duka zote ufilisike, nikamwambia kwanini tena unasema hivyo akajibu nakutania bhana.....

We nenda kachukue maelekezo unaweza ukawa mteja wetu, nikasema sawa ila mie akili ikawa inawaza niondoe na namba ya yule dada wa mapokezi tu manake kashanichanganya akili yangu πŸ˜„. Basi bhana nikarudi nimaliziwe kuelekezwa eeh bhana eeh nilichosikia nilichoka sana

Dada ananiambia kuna masaji ya laki na nusu hii ukifanyiwa kuna happy ending na laki mbili na nusu ni full body masaji na happy ending, ikabidi niulize happy ending ndo nini asee nikaambiwa kama mwanaume lijali unapogusana na mwanamke lazima hisia zipande....

Sasa huwezi kuvumilia zile hisia zinapopanda ndo hapo tunaamuwa kushusha hisia kwa happy ending nikaoona oohhh kazi ipo. Nikamwambia ila mie nataka masaji nifanyiwe na wewe na nipewe na happy ending inawezekana akajifanya kusema mie siruhusiwi sababu kazi yangu ni kupokea wateja

Nikaamzimgua nikamwambia sio hapa nataka uje unifanyie kwangu, akasema na mkeo jee mie sitaki ugomvi nikamwambia hadi nakuita kwangu inamaana ujue nipo single bibie we niambie tu inawezekana au vipi, akawa anadengua dengua na pozi za sitaki nataka nikamwekea simu akachora namba

Nikamwambia nitakucheki basi ili nijue ratiba zako ili tupange vizuri manake nataka hiyo happy ending iwe siku nzima nikaona anajichekesha chekesha pale kiaibu aibu nikajisema kimoyo moyo we cheka tu ila ukija mie maswala ya masaji sitaki nataka happy ending mwanzo mwisho πŸ˜„

Vipi wanangu mnanishauri nipige simu mtoto avuke geto au nikaushe manake mtoto anasifa zote za kuwa demu mkali asee kama mnavyojua trump misaada ya dawa kasitisha πŸ˜‚ au liwalo na liwe tu mie niivute niichape tu πŸ˜„

C&P.X
 
UZI WA KIJOBLESS.

Those day nilikuwa nadate na msichana mmoja hivi alikuwa anasoma chuo. Mimi nilikuwa nipo mtaani tu, tunaweza kusema nilikuwa jobless.

Kuna kipindi alikuja mdogo wangu nikawa naishi nae, huyu mdogo wangu yeye alikuwa hana mpenzi. Kila Mdada aliyekuwa anamtakaa alimkataa sio kesi.

Siku moja nipo nachat na mtu wangu. Tumuite Aneth. Wakati nachat na Aneth akawa ananambia yupo kwa rafiki yake anaitwa Esta.

Huyu Esta yeye alikuwa na mpenzi wake, lakini alikuja kugundua mpenzi wake anamcheat na Mdada mwingine wa chuo hicho hicho.

Sasa Aneth akawa ananambia amejaribu kumbembeleza sana rafiki yake asiwe mnyonge imeshindikana hajui hata afanye nini.

Akawa ameniuliza mimi, Mimi nikamwambia hapo kuna njia mbili. Moja akae atulize akili kwa mda ili awe sawa na mbili atafute mpenzi atakaemfanya amove on haraka.

Aneth akasema sasa huyu wa kumfanya amove on haraka atampata wapi.

Nikamwambia si unamjua huyu mdogo wangu, ni mtu poa sana alafu pia kasomea hayo maswala ya ushauri nasaha, wewe mlete rafiki yako huku kwa huyu amshauri chap atakaa sawa.

Kweli bhana akanipa namba. Kusema kweli huyu mdogo wangu ni janja janja tu hata hayo masomo ya saikolojia hayajui ni vile nilikuwa namtafutia demu.

Basi kweli wakaanza kuwasiliana, kumfariji. Ikafika kipindi wakakutana wakawa wanaenda kufanya mazoezi pamoja, kiufupi mara nyingi Esta akitoka chuo alikuwa anashinda na huyu mdogo wangu.

Siku, wiki na hatimae miezi ikapita wakawa wapenzi, na walishibana kweli kuliko mimi na Aneth.

Muda huu nawaandikia hapa ni kwamba mimi na Aneth tuliachana vibaya mno.

Kilichotokea ni kwamba yule jamaa wa Esta alitaka kurudi tena kwa Esta kuomba msamaha, akamtumia Aneth kumbe Aneth anampendaga yule ex wa Esta. Akatumia fursa hio kujiweka karibu na ex wa Esta na wakaingia kwenye mahusiano bhana me nikaachwa.

Kuhusu mdogo wangu na ESTA ni kwamba wiki ijayo ndio wanaowana.

Huyu mdogo wangu ni mdogo wangu kimtaa tu sio ndugu yangu.

Wakati tumeenda kuonekana kwa kina Esta, tuliwakuta wazazi wake Esta na ndugu wengi wengi tu.

Palikuwa na mtoto wa Bamdogo wake Esta, alikuwa anafanana umri na Esta, na hapo sio mda mrefu toka niachane na Aneth, maana Esta anajua kila kitu.

Wakati tunaondoka Esta alinifuata akanambia anashukuru maana bila mimi yeye asingekutana na mdogo wangu, maana Aneth alimsimlia mpango mzima ulivyokuwa.

Akanambia najua wewe ni Aneth mmeachana kwa sababu ya ex wangu, umemuona yule pale mtoto wa Bamdogo yangu anaitwa Janethe, najua unapitia kipindi kigumu ambacho nilikuwa napitia mimi kipindi kile VIPI NILIPE FADHILA......!!!

nikamuangalia yule mtoto wa Bamdogo Esta nikasema ila shemejiiiiii....... Tukawa tunaondoka huku tunachekaaa....

vipi wanangu mananishaurije FADHILA ILIPWE.., lakini kumbukeni anaitwa JANETH jina lake lenyewe linaanza na J

Pichani ni mimi baada ya kumuona JANETH

@highlight
 
Ipo hivi....

Wakati upo shuleni ulikuwa unaona mtaani fursa nyingi sana.Kipindi unasoma ulikuwa unaona wanaokaa mtaani hawana kazi ni wazembe sana

Sasa siku hizi wewe umemaliza shule upo mtaani hata zile fursa ulizokuwa unaziona pindi unasoma zimekimbiaπŸ˜‚πŸ˜‚ hadi unatamani ungekuwa na daftari uziandike ukimaliza shule uanze kuzishughurikia tuπŸ˜‚πŸ˜‚.

Saivi wewe ndo umekuwa unatafuta connection kuliko connection yenyewe

Kitu ambacho ulikuwa hukijui kipindi hicho ni kwamba.....

Maisha ni kama ndoa tu.Walio ndani ya ndoa wanaona mabachera wanafaidi wakati mabachera wanaona walio oa wanafaidi.hapo kila mtu anaona mwenzake anafaidi kama wewe unavyoona wanafunzi wanafaidi saiziπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

NB;Wale tuliolingana umri punguzeni kufanikiwa wanangu jamii inaniona Mimi Mzembe hukuu

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
 
Chai
 
Dah jf sikuhizi inaboa sana, yote haya ameyakopi Facebook anakuja kutuletea huku. Sas kuna utofauti gani wa facebook na jf
 
Kwakuwa trump kastisha,na we achana na hizo mambo,utayavagaa bure,ubaki unajuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…