Mwaka 2000 ndo tumehitimu formIV.
Jamaa yangu wa kitaa yeye alikuwa kagraduate seminary tupo wote tunasikilizia results.
Jamaa alikuwa na mahusiano na kabinti flani katoto ka mchagga mmoja mbabe sana halafu mbesa kwake ipo na ni meneja karakana flani ya kuchakata mbao.
Mara kidogo results zikawa zimetoka, na wote tukawa tumefaulu safi tu yaani kwenda advance uhakika!
Sasa kadri siku zilivyoenda, jamaa nikamwona hana mzuka furaha imekata kabisa.
Kumuuliza, ikabidi anifungukie kuwa kale kabinti kakaharibu kakatia mimba ndiii!
Anahofia itakuwaje parokiani wakijua na yeye lengo lake ni kuwa padre!
Mbaya zaidi mchagga ni katili anamiriki pa pa paaa!
Ikabidi tudraft mkakati wa kuichoropoa kabla mchagga hajasanuka!
Tukaenda kituo cha afya kumcheki dada flani akatuuzia pills za abortion.
Mimi nikampelekea yule binti na nikampa maelekezo yote.
Tukatulia kama wk2 kusikilizia kama mpango umetiki.
Nikaenda kumcheki binti akanijibu hajaona kitu!
Ile kumpa feedback jamaa akaanza lawama kuwa sijamuelekeza demu vizuri.