Uzi wa kupeana machimbo mbalimbali ya vifaa vya ujenzi na bei zake

Cement ya 42 ile kali inauzwa mtaani 17,500 na kuniletea mpaka home niongeze buku. Kuna jamaa nlimuona Facebook anajiita Michael Ngus aliniletea mpaka saiti Kwa 15,500 sharti tu uchukue kuanzia mifuko 100
Itakuwa upo Ujenzi Zone πŸ˜ƒ
 
Kwenye mbao ulipigwa.
Maana mbao nzima ya ft 12 ni 2500/=
Eq ya Tsh 200/ Ft 2by2

The same kwenye 4by2
 
Cement ya 42 ile kali inauzwa mtaani 17,500 na kuniletea mpaka home niongeze buku. Kuna jamaa nlimuona Facebook anajiita Michael Ngus aliniletea mpaka saiti Kwa 15,500 sharti tu uchukue kuanzia mifuko 100
Habari.Unaweza nipatia namba ya huyo jamaa.?
 
Hapo kwenye mbao, je ni mbao zenye dawa au zimepigwa rangi ya ukili? πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸš¬πŸš¬πŸš¬
 
ukiona unauziwa mbao kwa futi ujue umepigwa. Mbao za kuezekea nunua 4 x2 za futi 12 kwisha kazi
Inategemea, mimi nilikutana na jamaa ambae anakwenda kuchukua mzigo mwenyewe Iringa, alinishauri ninunue za 2x6, 2x4, kisha nikachanisha kupata 2x2, gharama ya kuchana ni juu yake na mbao zimepigwa dawa urefu ni zaidi ya futi 18. Alinisimulia kwenye uvunaji kunakuwa na mbao za aina mbili na zote zinaingizwa sokoni. Za Serikali miti inakuwa imekomaa na zinakuwa zimepigwa dawa. Na zinazovunwa na wanakijiji nyingi miti inakuwa haijakomaa na hazijawekewa dawa, hivyo pale Buguruni huwa wanawalangua kwa kuwapigia rangi ya ukili (kijani)
 
Hii bati ya sh 11,500/ ni ya rangi au haya kawaida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…