Uzi wa kusimulia sehemu nzuri uliyowahi tembelea na mazuri ya kushangaza uliyoshuhudia huko

Uzi wa kusimulia sehemu nzuri uliyowahi tembelea na mazuri ya kushangaza uliyoshuhudia huko

Utalii wa ndani, nilienda sehemu moja inaitwa maji moto mkoa wa Katavi. Ni ka-mto kadogo maji yake ni ya moto (si sana) yanafaa kuoga kwa sehemu za baridi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanga nilipenda sana daladala za baiskeli unataili barabara zote 21, maisha yao ya mtaani pia ni maisha ya kurizika wanashukuru kwa wote.

Rombo niliwai fika kule nilifurahia mbege fresh na nyama za pori

Arusha nilipenda sana kipindi cha amu iliyopita unaweza fika bar watu wakafika mezani kwako mkaanza kula bia zisizo na idadi ,wakamaliza wakalipa na kusepa

It is never to late to begin. Start now
 
Kwa kweli Tanga nami ndo mara ya kwanza kukuta daladala ya baskeli na ndi mara ya kwanza kupanda maishani kwangu.
Nikaja kuzikuta tena Geita wanaziita "daladala"

Ushirombo kule Katente, nilitembelea Kashelo hadi Lyambamigongo ndanindan huko.....
Kwakweli sijawahi pata locations poa kama zile...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli Tanga nami ndo mara ya kwanza kukuta daladala ya baskeli na ndi mara ya kwanza kupanda maishani kwangu.
Nikaja kuzikuta tena Geita wanaziita "daladala"

Kwa tanga inavutia maana unafanya utalii wa ndani kwa haraka

It is never to late to begin. Start now
 
~ kuna kijiji nilipita nilikuwa natoka geita kwenda kahama ndani ndani niliona uwanja Wa mpira Wa miguu unanyasi za kijani sana halafu size moja kama uwanja Wa Wembley na majukwaa yake yamejengwa vizuri kwa kutumia mbao...nilishangaa sana kuona ubunifu kijijini sana,wakati dasalam wanachezea mpira kwenye matrip ya mchangaa!!!
 
Kwa kweli Tanga nami ndo mara ya kwanza kukuta daladala ya baskeli na ndi mara ya kwanza kupanda maishani kwangu.
Nikaja kuzikuta tena Geita wanaziita "daladala"
Shinyanga,nzega.....n.k
 
Lindi- mtwara
IMG_20200328_080931.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkoa wa Tanga:Nilipata kutembelea sehemu mbili Wilaya ya Lushoto na Bumbuli.

Tukianza na Bumbuli kuna msitu unaitwa Mazumbai ile sehemu ni utalii tosha mahali pale kuna sehemu walishawahi ishi wazungu miaka zaidi ya 50 iliyopita hivyo kuna kota wameziacha pale na ni gharama kidogo sana kulala zile kota.

Madhari ya msitu wa mazumbai na eneo lile hustaaabisha sana Maana kuna historia na mambo mengi yanayovutia mahali pale:Maji masafi yanavyotirika,Mashine za kufua umeme,Uwepo wa miti mingi mirefu na msitu uliojazwa na kila aina ya nakshi na jambo zuri husimamiwa na chuo cha Sokoine hvyo kufanya uzidi kuvutia zaidi,Ule ulikuwa utalii wa ndani hasa.!

Wilaya ya Lushoto mjini kabisa: ukipanda juu utakutana na Irente view ambayo imejengwa nafikiri ni kwenye mwamba na kuna hotel safi iliyokaa kitalii na yenye kuvutia,

Ukiwa pale Irente ukiangalia chini unaona Barabara inayoelekea Same,

Hzi sehemu mbili nitarudi siku moja..!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom