Keagan Paul
JF-Expert Member
- Jul 19, 2018
- 510
- 3,178
Ilikuwa mwaka 2012, Mara yangu ya Kwanza kufika Beit Bridge, Mpaka wa Zimbabwe na South Africa, Ilikuwa saa nane usiku. Ilikuwa safari ya Siku tatu kutoka Dar hadi kufika hapo. Ndani ya Bus tulikuwa tumechoka sana. Bus lilikuwa na raia wengi wa Zimbabwe na Zambia, Waburundi, Wakenya. Wabongo tulikuwa 4 tu. Wabongo tulipiga mastori kibao, kama watu tuliofahamiana miaka mingi, kumbe ndo ilikuwa Mara yetu ya kwanza kukutana.
Tulijichanganya sana na Waburundi na Wakenya. Wazimbabwe hata Lugha yao tulikuwa hatuelewi. Dah ilikuwa moment fulan tamu sana.
Pale border mbongo mmoja hakuruhusiwa kuingia South Africa. Alikamatwa alitaka kutoa rushwa kwa Afisa wa Uhamiaji (Mkaburu) ili apewe miezi 3 ya kuishi Kwa Mabida.
Sisi wengine tuligongewa muhuri wa mwezi 1 tu kuwepo kwa Madiba. Lakini tuliishi zaid ya Miaka 6. Sio Miezi 6, Ni miaka 6. Harakati za Mtu Mweusi bhana.
Nakumbuka wabongo wote tulienda kufikia Pretoria kwa jamaa fulani. Kumbuka wote hapo hatujuani, halafu mfukoni nimebakiwa na kama Elfu 50 tu ya kibongo.
Kati ya sisi tuliotoka Bongo, kuna mwenzetu mmoja anafamiana na huyo jamaa tuliyefikia kwake. Jamaa wa kuitwa Ibra, alitupokea vzr sana.
Tulikutana na wabongo Kibao pale Pretoria, Walituchukua Maelezo, tulikutana mpaka na yule demu video queen wa Matonya, wimbo wa Vailet, demu south africa bado wanamuita Vailet, bado mrembo sana.
Harakati za kuingia Mtaani kusaka Mishe ndo zikaanzia hapo.
Nilikaa pale ghetto kwa washkaji kama wiki mbili ivi, ndani ya hizi wiki Mbili na jamaa zangu tulikuwa tunaenda sana Johannesburg. Mwenyeji wetu alikuwa na rafiki zake wengi huko.
Johannesburg na Pretoria sio mbali sana, kwa daladala ni kama dakika 40 tu.
Basi bhana
Katika kwenda kwenda Johannesburg siku mmoja kwenda Daladala nikawa nimekaa na demu mmoja mkaliii, nikawa namsemesha semesha Mara pap akanipa namba yake ya Simu. Washkaji zangu wananichora tu.
Mademu wa South Africa wakitongozwa sio wagumu sana kama Dada zetu wa kibongo, siku ya pili demu akawa demu wangu, fasta tukaanza kupanga maisha Ha ha ha ha
Demu anafanya Kazi Bank FNB, pale Midrand njia kama unataka kuelekea Kalfonteen. Baada ya kama siku 4 toka tufahamiane na yule manzi tukaanza kupiga story za jinsi ndoa yetu itakavyokuwa. Jinsi atakavyokuja bongo kukutana na ndugu zangu, alivyoleta tu stori zake za siku moja atakuja Bongo kukutana na ndugu zangu, mtu wa kwanza kumuwaza alikuwa Mama Riziki, Jirani yetu Buza, atakavyoongea mtaa mzima.
Yaan mm na yule demu ilikuwa ni full uongo uongo tu mpaka demu akajaa. Akaamini kabisa kama kweli mm ntamuoa.
Zote hizo ni Harakati za Mtu mweusi katika kutafuta sehemu ya kuanzia.
Mara siku akanipigia simu akaniambia kwa Kingereza 'Keagan nataka tuishi wote'
Dah
Sent using Jamii Forums mobile app