Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Uzi wa Matembezi (Travel & Vacations) na Vivutio vya Utalii nchini Tanzania

Wasalaam,

Ni imani yangu mu wazima wa afya, kama kichwa cha uzi huu kinavyosomeka, lengo la uzi huu ni kushare experience ya matembezi katika maeneo tofauti tofauti ya kuvutia na vivutio vingine vya utalii vinavyopatikana nchini kwetu tanzania.

Tuanze,
Matembezi, Ziara ni nini?

Neno Ziara ni nomino inayoashiria kutembea ama kuzuru mahala fulani, unaweza kutembea ndani ya mipaka ya nchi yako ama nje ya mipaka hiyo, (tutajadili kuhusu ndani ya nchi yetu). Ziara inaweza kuhusisha mtu mmoja ama kundi la watu mfano familia, marafiki, wapenzi n.k.

Katika historia ya mwanadamu Ustaarabu ama utaratibu wa kuzuru, kutalii ama matembezi yalianza huko ughaibuni magharibi mwa nchi za ulaya, ambapo historia inazungumza baada ya mwanadamu kuwa na ziada ya mapato yake (surplus) alianza kuridhika na kutafuta shughuli nyingine tofauti na uzalishaji mali, hapa ndipo idea ya kutembea na kutalii ilipokuja.

Ingawa historia zinaonyesha ziara/matembezi yalifanywa na mataifa mengi hapo kabla hasa kwaajili ya kufanya biashara na mataifa mengine ya mbali, na hapa ndipo tunapata aina mbalimbali za utalii. Utalii/Ziara zimegawanyika katika makundi tofauti hasa kutegemea lengo la ziara yenyewe, hapa tunapata

[emoji1635] Ziara kwa ajili ya burudani (leisure purposes ) ; hapa watu husafiri kwa ajili ya refreshment na kusherehesha mwili na akili.

[emoji385] Ziara kwa ajili biashara (business purposes ) ;hapa watu husafiri kutoka sehemu moja ama nyingine kwaajili ya biashara na wakati huo huo anatalii.

[emoji432] Ziara kwa ajili ya masomo (Education purposes) wapo wanaofunga safari kwaajili ya kwenda kujifunza mambo mbalimbali i.e kihistoria, kitamaduni n.k

[emoji381] Ziara kwa ajili ya matibabu (Healthy purposes) Hii wengi hutokea bila ridhaa zao lakini wapo ambao wana plans za kusafiri let's say abroad kwaajili ya check up kila mwisho wa mwaka at the same time wanaenjoy.

Makundi ya utalii yameenda mbali zaidi mpaka tumepata aina kama utalii wa ngono (sex tourism) hapa kuna watu wanasafiri sehemu tofauti tofauti kwaajili ya kukidhi matakwa ya kingono.


Matembezi/ Utalii/ Ziara na Watanzania

Hii naweza kusema ni changamoto kwa jamii zetu za kitanzania, wengi wetu tumekuwa hatuna utaratibu wa kutoka, kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwaajili ya kutalii/ kujifunza n.k watanzania (wengi wao sio wote) tuna uvivu wa asili wa kusafiri, inafikia kipindi mtu anaenda kikazi nchi za nje anakutana na mzungu anamuuliza kuhusu let's say kilimanjaro, serengeti mbongo anabaki kucheka cheka tu au ataishia kudanganya kanakwamba ana experience ya hizo sehemu kumbe anaishia kuona tu kwenye Tanzania Safari Channel.

Hii si kitu kizuri, wengi wanaweza kujitetea kuwa may be kutokana na gharama za usafiri wa kufikia maeneo husika lakini hebu tujiulize ni kiasi gani baadhi yetu tuna spend let's say ulabu ama kuvaa lakini mtu anaishi Tanga ila magoroto anapasikia tu ama kuona instagram [emoji36].

Well may be inaweza kuwa Matembezi/Kusafiri ni hobbies kama hobbies nyingine ambazo wengine ni starehe kubwa sana kwenye maisha yetu while kuna mtu anakushangaa kuspend pesa kwenye kutalii lakini napenda kutumia nafasi hii kuwa encourage wan JF tupende kutoka, tupende kutembea hata wewee uliye business oriented you never know utakutana na nani kwenye matembezi yako, si kila madeal yanapatikana bar tu [emoji23][emoji23].

Turudi kwenye lengo mahsusi la uzi wetu, let's share experience mbalimbali na maeneo mbalimbali ambayo either umewahi kutembelea ama una mpango wa kutembelea kwaajili ya kuhamasisha wengine ambao hawakuwa na utaratibu au kupenda kutembea.

Ukiachana na mbuga za wanyama ambazo naweza kusema nyingi ni well known Mimi nitaanza na, maeneo haya yafuatayo, karibuni.

Baadhi ya Vivutio

Lushoto Tanga

Magoroto Forest Muheza

Kikuletwa Hot Springs Moshi

Lake Chala, Moshi

Uluguru mountain

Mt. Uluguru Morogoro

Caravan serai, Bagamoyo

Mwonekano wa mlima Kilimanjaro kutokea Lyamungo Machame

Gombe National Parks, Kigoma

Uduzungwa National Parks, Morogoro

Mombo, Tanga

Msitu wa Njombe

The Overhang, Kigamboni

Lushoto View Point, Tanga

Katavi National Park, Katavi

Tarangire National Park Arusha

Saadani national park Bagamoyo

Ngorongoro crater Arusha

Ziwa Victoria, Mwanza

Mataruni waterfall, Uru Moshi

Potwe potwe(Papa Potwe) Kisiwa cha Mafia



Sent using Jamii Forums mobile app
Saa nane Mwanza
Kitulo natural garden
Lake Ngozi Mbeya
Kijungu Kiwira
Kiteputepu bridge and valley
Isimila pillars
Mikumi NP
Selous
 
IMG_6503.jpg
 
IMG_6655.jpg


Muda wa "Kadansee" na muziki laini, Cape Town Fish Market, Znz.
 
Kwetu ni kuzuri.
Hapo Mambo kijiji kiko ng'ambo ya mlima.
Tunapita kuelekea Irente huko na Mtae
Irente sikufanikiwa kufika ila next time i will, nilipita Mtae na nilifikia Mambo view lodge, nilikaa siku sita, aisee ukiacha baridi kali iliyokuwa ikinisumbua nilitamani nikae zaidi pale mambo, mandhari mazuri sana na yakuvutia.
 
Irente sikufanikiwa kufika ila next time i will, nilipita Mtae na nilifikia Mambo view lodge, nilikaa siku sita, aisee ukiacha baridi kali iliyokuwa ikinisumbua nilitamani nikae zaidi pale mambo, mandhari mazuri sana na yakuvutia.
Kabisa.
Sema kwa msimu huu ujao kwetu Malindi hakukaliki, ni baridi sana, sana.
Karibu tena siku ingine ukija nitakupa zawadi ya mboga za majani zinaitwa "mbwembwe" na matunda yanaitwa Mafyoksi..na makakala.
 
Kabisa.
Sema kwa msimu huu ujao kwetu Malindi hakukaliki, ni baridi sana, sana.
Karibu tena siku ingine ukija nitakupa zawadi ya mboga za majani zinaitwa "mbwembwe" na matunda yanaitwa Mafyoksi..na makakala.
😂 😂 I will kwakweli nazisubiri hizo "mbwembwe" kwa hamu.

Niliona namna wakina mama wakilima mboga za majani, pilipili hoho na viazi mviringo kwa wingi, inaonekana rutuba ya kule ni nzuri sanaa.
 
😂 😂 I will kwakweli nazisubiri hizo "mbwembwe" kwa hamu.

Niliona namna wakina mama wakilima mboga za majani, pilipili hoho na viazi mviringo kwa wingi, inaonekana rutuba ya kule ni nzuri sanaa.
Kule rutuba ni rafiki sana na mazao.
Vitivo vimestawi mno.
Na kuna maji ya kutosha.
I wish ningekuwa nyumbani sahv, niko jikoni nachemsha magimbi huku babu anamkamua ng'ombe maziwa.
Ngoja nitafute picha nikizopiga kwetu nikuoneshe
 
Back
Top Bottom