Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Wewe Mtu Nyanya Chungu unaijulia.

Siku zote Nyanya Chungu inaendana na Bamia.

Sema nimegundua Nyanya Chungu yako unapenda kuimenya.

Hebu siku nyingine ipike na Maganda yake ili upate kitu roho inapenda.


img_20170815_122946-jpg.566653
Msombe wa nyanya chungu za kuchoma, limao na pilipili ulishakula?
 
SUPU YA MAKONGORO

Mahitaji

-Makongoro (miguu ya ng'ombe) kiasi
-Limao 1 kubwa
-Kitunguu swaum
-Tangawizi
-Chumvi
-Pilipili

Matayarisho

Safisha makongoro kisha yatie kwenye pressure cooker au yapike kwenye jiko lolote.

. tia kitunguu swaumu, tangawizi, chumvi,limao na maji kiasi. Baada ya hapo yachemshe mpake yaive na yawe malaini na pia ubakize supu kiasi inaweza kuchukua kama dk 45 au saa 1 hivi.

Baada ya hapo yaipue na upakue supu yako kwenye bakuli katia pilipili kiasi kisha itakuwa tayari kwa kuliwa.

Note:
Ukiwa unanunua makongoro hakikisha unachukuwa yale yasiyokuwa na manyoya na pia
hakikisha usiyachemshe kupitiliza kwani yakiwa malaini sana utashindwa kuyaenjoy.

Screenshot_20211219-131324.jpg
 
Back
Top Bottom