Uzi wa vyakula tu

Ah kumbe uji ndo unachanganywa kiivyo eeh?. Asante sana ngoja na Mimi nijaribu tena. Maana nahisi nilikosea kwenye kuchanganya.

Halafu pale kwnye kuisaga sukari na mwiko. Mbona huwa haisagiki kabisa na Kwa haraka. Kwanini?. Au nyie mnaisagaje?
Jitahidi tu kukoroga sana.
Blueband na sukari,,inasagika.


Ndiyo,nachanganya Kwa nguvu kama nasonga ugali.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Hizi nazipendaga lkn zinajua kutoka ngumu balaa
Ukitaka kupika chapati nzuri za kusukuma lazima uwe mpole,usiwe na haraka.
Ukifanya haraka haraka lazima utoe chapati ngumu.

Kanda vizuri hadi upate ule ulaini unaoutaka.


Funika,kama dakika 15 hivi...sehemu yenye joto.

Baadaye unaendelea..
Mimi nikishasukuma mara ya kwanza nikatengeneza maduara ya mikunjo,huwa nafunika tena ili zilainike zaidi..
Nikifunua hapo naanza kusukuma sasa Kwa ajili ya kuzipikaa.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…