Lizzy sijawahi kuandika chochote kuhusu wewe ama mapishi yako.
Wakati wote huwa na observe tu.
Pamoja na sifa nyingi za watu wanazokupa humu kuhusu kupika na kula chakula kidgo ila sifa yako moja kubwa inayonipendeza kwako ni USAFI NA MPANGILIO.
Nadiriki kusema wewe ni msafi/nadhifu mno jikoni kwako na nadhani hu msafi kwa jumla na upo unajua kupangilia kila kitu kikakaa mahali pake.
Kila picha yako unayo post natizama utakuwa jiko safi, sahani safi, microwave safi hata nikitizama chini kwenye tiles naona kuna ngaaa.
Unastahili pongezi mnoooo.
Napenda sana mnoo mtu wa hivi.
Siku zote huwa na observe na kufurahi moyoni ila leo nimeamua kukupa sifa zako.
Bila shaka observation hii wamefanya wengine pengine hawajapata muda wa kukusifia tu, ila naamini wote wataungana nami.
Kwa kweli dada
Lizzy nakutunuku shahada ya juu ya heshima ya usafi na mpangilio mzuri honoris causa(Phd in sanitation and good arrangement honoris causa)
Hongera Dr.
Lizzy phD