Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Hongereni kwa vyakula vizuri na lishe bora viongozi, inapendeza kuona hali ya upishi na usafi wa hali juu. 👏

Samahani naomba recipes za aina ya mboga inayoweza kutumika na chapati ukiachia maharage. Recipes zizingatie sio mtumiaji wa nyama, samaki, dagaa na bidhaa za wanyama.

Shukrani. 🙏
Mboga nyingine unaweza pika mboga ya majani yoyote unayopendelea isipokuwa tembele na mlenda.

Kuzipika kwakwe ili zinoge na chapati usipike kama tunavyopika mboga za majani za kula na ugali. Hapa ili zinoge unaziunga kama tunavyounga mchuzi wa nyama au samaki.

a)Unaziunga kabisa, kaanga kitunguu kidogo, add garlic/ginger iliyosagwa kiasi, add nyanya iliyokatwa na nyanya paste kama utapenda, add mboga zako tia tui zito la nazi au nazi ya pakiti, koroga kupata sotojo. pika nazi iive tayari kwa kuliwa.

b)sotojo la uyoga. Process zake za kupika kama unapika mboga zingine zozote.
 
IMG_0194.jpg

Show timeee!
 
Okay ile hayako popular kule hayo.
Kuna baadhi ya mazao Mbeya wanaringa kula,yaani ni vyakula vya mifugo.
Kuna ndizi ilikua inaitwa harare walikua hawali kabisa wanatupia nguruwe.

Mkuu mbeya wana aina nyingi sana ya vyakula nna plan za kuhamia huko pia napapenda sabahu ni karibu na hometown sumbawanga ukiwa mbeya una 1000 mfukoni unakula unashiba.
Ukienda pale mbalizi kuna kila aina ya maharage unayoyajua wewe.
 
Hapana Hayo ni meupe Kama njugu
Okay ile hayako popular kule hay
Hongereni kwa vyakula vizuri na lishe bora viongozi, inapendeza kuona hali ya upishi na usafi wa hali juu. 👏

Samahani naomba recipes za aina ya mboga inayoweza kutumika na chapati ukiachia maharage. Recipes zizingatie sio mtumiaji wa nyama, samaki, dagaa na bidhaa za wanyama.

Shukrani. 🙏
Chapati tembele jaribu lete mrejesho😁.
Dengu,mbaazi la nazi
 
Habari..

Sisi kuna menu huwa tunaenda kula kwenye mgahawa mmoja wa kihindi, inaletwa hiyo curry na chapati au Naan. Siku moja nikamuuliza chef inavyopikwa akanielekeza sababu tumezoeana sana, na i went to try ikatoka perfect.

Recipe:
Dengu iliyochemshwa kiasi
Nyanya moja.
Kitunguu maji kikubwa
Garlic punye 3 au 4.
Viazi mviringo vikubwa vi3
nyanya paste kijiko cha chakula 1.
Tangawizi mbichi kijiko cha chai 1.
Paprika kijiko cha chai 1
manjano ya unga kijiko cha chai nusu. (kama unapendelea)
Curry powder kijicho cha chai 1 (kama unapendelea)
Nazi 1.
Chumvi kiasi.
Cauliflower kiasi.
Pilipili zile ndefu za kijani 2, ndefu nyekundu 2, na mbuzi moja. (pilipili unaweka kwaajili ya harufu hivyo usizipasue hata kidogo)
Majani ya giligilani au majani ya kitunguu. (option)

Kupika. Process yake ni kama ya kuunga nyama au mchuzi wa aina yeyote.

Kaanga kitunguu kisiwe cha brown, add garlic+Ginger, then add nyanya iliyokatwa katwa koroga ikikaribia kuiva add nyanya paste na viungo vyote vya unga unavyoenda kutumia, add viazi korogo koroga kabla havijaenda kuiva weka dengu yako, weka na cauliflower angalia zisijevurugika. acha viive kidogo weka tui lako la nazi na ka chumvi, pambia kwa juu na pilipili zako ambazo hazijapasuliwa na majani ya vituunguu au majani ya giligilian. Then wapakulie wajilambe na chappat zako.

NB. Cauliflower na viazi lazima zionekane ndio tunazila kama nyama, yaani tonge nyama.
Asante, nitakuja jaribu hii.

Asante kwa recipes zote na ya pili nimepokea pia.

Napenda sana kupika na vyakula vyangu ni very limited hivyo inanifanya kubadili mara kwa mara au kubuni pishi jipya.
 
Oh! Asante Lizzy

Pengine nimewasilisha vibaya, lakini namaanisha situmii nyama na viumbe hai vingine. Hata likes nakupatia kwenye vyakula visivyo na wanyama. 🥹

Great recipe though, naamini wengine watanufaika. 🙏
Geeez....I completely missed that part!!🫣🫣

Hongera kwa kufanikiwa kutokula nyama/samaki, mie nilishawishiwa ila tamaa ikazidi nguvu.🙈

Jaribu Green Peas, Choroko, Chickpeas (Njugumawe), Lentils (Dengu) ambazo zote unaweza kuchemsha tu kisha ukaunga kitunguu na nazi tu. Siku ukitaka kubadili ladha ongeza hoho & carrot. Siku nyingine weka curry powder kunogesha zaidi. 🥥 isiwe inakosa!
 
Asante nitazingatia hii milo sasa.

Maharage yamekuwa ndiyo mboga kuu ikufutiwa na mboga za majani na irish potatoes.
 
Oh! Asante Lizzy

Pengine nimewasilisha vibaya, lakini namaanisha situmii nyama na viumbe hai vingine. Hata likes nakupatia kwenye vyakula visivyo na wanyama. 🥹

Great recipe though, naamini wengine watanufaika. [emoji120]
Hauli nyama?[emoji15]
 
Back
Top Bottom