Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Mi bado napambana kulipika ila sijafanikiwa. Napenda biriani kuliko ninavyopenda wali samaki. Siku nikilipatia sijui itakuwaje.
Hapo naendaga kula ijumaa kwa Sele bonge

Mimi nimefanikiwa ila nachemka kwenye mtindi ,kila nikiweka mtindi kwenye mchuzi unakua kama unakatika.
 
Kingine unaweka maziwa gani? Maana niliambiwa plain yoghurt nikatafuta nikakosa nikaweka hizi yoghurt za dar fresh.. ila nimeona plain yoghurt Village Supermarket nitanunua nipike na ile nione kama yatakatika tena
Niliambiwa papai sikutaka hata kujua wanatumiaje maana vya kuweka papai kwenye mboga siviwezi.
 
Kingine unaweka maziwa gani? Maana niliambiwa plain yoghurt nikatafuta nikakosa nikaweka hizi yoghurt za dar fresh.. ila nimeona plain yoghurt Village Supermarket nitanunua nipike na ile nione kama yatakatika tena

Niliambiwa mtindi tu wa kawaida ila mzuri zaidi wa Iringa.

Uniletee mrejesho
 
Unajua tui la nazi likimwa limekatika?ndo hivyo yaani unaona kama vidude vyeupe vyeupe.

Nishapika mchuzi kabisa mtindi unakua wa mwisho.
Sasa huko sio kukatika my dear.

Pia inategemea na kiwango inachoweka huo mtindi.

Kma ni wa kupika nyumbani au chakula cha watu wengi.

Bora masalo yako yawe na ladha ya viungo tatizo ni kwenye makisiaji ya viungo na masalo kuchemka vzuri.
 
Kukaya vino chavitanga vimanda....! Usekuuza umwile....
tapatalk_1541322870558.jpeg
 
Back
Top Bottom