Uzi wa vyakula tu

Naomba recipe ya hizo tambi zimenivutia

Sent using Jamii Forums mobile app

Ngoja nikupe yangu mim ambavyo hupika
Naweka mafuta yanamcheka ,nakaanga tambi natia hiriki na sukari kiasi na chumvi kiasi
Tambi ikiwa ya brown naweka maji kiasi (unakadiria kutokana na aina ya tambi zenyewe)
Nikiona maji yameanza kukaukia na tambi zimelainika natia nazi kisha nazigeuza ili nazi ishike tambi zote
Hapo napunguza moto uwe mdogo au kama kuna jiko la mkaa lina moto unabakisha makaa ya moto kidogo unabanika unaacha kama dakika moja tu unatoa

Sio lazima tambi kuzikaanga unaweza kuzichesha tu zikiiva tia nazi ,hiriki,kama unapenda sukari tia na chumvi kama hupendi weka chumvi tu

Pia kuna za kuchanganya na nyama unachemsha tambi zinaiva ,kisha nyama iliyochemshwa unairosti hakikisha inaiva vizuri kabisa(usisahau karoti ,hoho, mim hupenda kuviweka mwishoni ili zisiive sanaa, kisha unachanganya kwenye zile tambi zako unapunguza unaacha inaiva taratibu huku unazigeuza Kwa muda kadhaa unaipua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…