Uzi wa vyakula tu

Napenda sana pilau... Hasa kuila JumaPili mchana na usiku
Unatakiwa ule chakula kinachohitajika na mwili wako katika kuimarisha afya ya mwili,kinga ya mwili pamoja na kupambana na magonjwa mbalimbali na wala siyo kula chakula unachotaka/unachotamani wewe.

Katika kuimarisha afya yako ya mwili unahitaji kula majimbi,viazi vya aina zote vilivyochemshwa,mihogo iliyochemshwa,nafaka zisizokobolewa,matunda,mbogamboga za majani, nuts za aina zote kama vile karanga,maziwa,mayai na kadhalika.

Jifunze kula kile ambacho mwili wako unahitaji katika kuimarisha afya ya mwili wako na wala siyo kula kile unachotamani wewe.Kumbuka unaishi mara moja tu kwa hiyo ipe afya ya mwili wako kipaumbele.Tunaangamia kwa kukosa maarifa.

CC:kwa mpenda pilau mwenzako Saint Anne
 
Pilau huwa nakula J2 tu.
Mboga za majani karibia kila siku mchana nakula..
Viazi,majimbi ndio kifungua kinywa..labda hapo kwenye matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jitahidi kula matunda sasa na ule ugali wako pendwa wa sembe achana nao na pia punguza sana kula wali.
Hapo kwenye wali Sasa[emoji23]
Ugali nakula ule wa mahindi yaliyolowekwa .
Matunda kwangu ni changamoto..napenda parachichi tu!
Ila tangu jana nameza malimao na machungwa kama Sina akili nzuti..homa imenibana kimtindo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji28][emoji28][emoji28]

Nashukuru kwa darasa mtaalamu

Vitu vyote vimetolewa ili vipokewe kwa shukrani...
 
Pilau huwa nakula J2 tu.
Mboga za majani karibia kila siku mchana nakula..
Viazi,majimbi ndio kifungua kinywa..labda hapo kwenye matunda.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jitahidi kula matunda sasa na ule ugali wako wa sembe achana nao na pia punguza sana kula wali
Hakuna chakula ambacho ni janga katika ulimwengu huu kama ugali uliolowekwa.

Ripoti za kitaalam zinadai kuwa mikoa inayoongoza kwa kuzalisha vyakula kwa wingi kama vile Mbeya ndiyo inayoongoza kwa udumavu kutokana na tamaduni zao za kula vyakula vilivyoharibiwa kama huo ugali wa kuloweka pamoja na ukosefu wa elimu/maarifa.Amka sasa achana na huo ugali wa kuloweka kwani virutubisho vyote humagwa chini au kuharibiwa kabla ya chakula kuliwa.
 
[emoji134]
Kwahiyo tule dona???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…