Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Chinese Fried Rice 🔥
Screenshot_20210516_152123.jpg


Screenshot_20210516_152052.jpg


Screenshot_20210516_151945.jpg


Screenshot_20210516_151926.jpg


Screenshot_20210516_151909.jpg


Screenshot_20210516_151851.jpg


Screenshot_20210516_151753.jpg


Screenshot_20210516_151631.jpg


Screenshot_20210516_151541.jpg


Screenshot_20210516_151519.jpg
 
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]hebu naomba break down

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekiiba lakini ntajaribu kukieleza kisela sela hivi... 😂
Kwanza chukua mayai 2-3,vunja kwa kisahani na uongeze chumvi na masala kiasi, koroga na umwage kwenye pan iliyona mafuta ya kupikia moto tayari. Yasikauke sana, kuwa unayatawanya kuwa vipande vidogo, then epua na uweke kando.
Chukua Ham 🥩 au steak yeyote uitakayo na ukate vipande vidogo kama cube za royco vile, kisha weka kando.
Chemsha mchele mwembamba hadi uwive, kisha epua na umwae maji yote na upoze tena kwa maji baridi huo mchele. Hii inaufanya usiendelee "kujipika" wenyewe. Kisha weka kando.
Chukua vitunguu maji vya vijiti katakata weka kando. Alafu ukiwa na peas, corn 🌽 Na caroti zilizochemshwa tayari, itakuwa safi sana 😬.

Sasa tuanze kupika - Chukua Pan kubwa, weka mafuta ya kupikia, yakiwa moto, weka sliced ham(ama steak uliyotumia) kwa pan, koraga hadi ziwe zinataka kubadili rangi hivi, ongeza mchanganyiko wako wa carrot, peas na corn 🌽, koroga zichanganyike vizuri. Chukua ule wali mkavu, changanya pia na uumwagie Soy sauce kiasi, changanya wee 😁. Baada ya dakika moja weka vile vitunguu maji ulivyokata kata na yale mayai vipande, na uendelee kuchanganya hadi vichanganyike vizuri. Hakikisha moto ni wa medium, wenye kutumia jiko la makaa, mfunge mlango wa jiko 🙄.
Kitu kiko tayari hapo lakini waweza ongeza kiungo chochote kile extra ukipendacho. Hapo mjomba kaongeza vipande vya kuku choma juu. Haya pakua kwa lile sinia uanze kuvurunya... Ishaisha iyoo!!! 👌
 
Back
Top Bottom