Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Samaki wa Nazi, Nyanya chungu, Bamia, Pilipili Hoho.


2939555_20210923_215732.jpg
 
Njoo unywe, tena haya huna nayagandisha mwenyewe, matamuuuu bakuli lake la kugandishia safiiii 😀

Halafu buana umeacha kupost misosi na wewe huwa unatusababishia majanga hasa kama mtu uko sehemu hakuna chakula 😀
Bora hata nimepata mwalimu, naomba nielekeze jinsi ya kugandisha maziwa nimechoka kudoea kwa watu☺
 
Bora hata nimepata mwalimu, naomba nielekeze jinsi ya kugandisha maziwa nimechoka kudoea kwa watu☺
Bila shaka bila shaka.

Simply nunua maziwa fresh ya ngombe ambayo hayajatiwa maji, chuja katika sufuria chemsha na yaache yapoe. Ukihakikisha yamepoa kabisa chuja katika bakuli safi then tia chachu, (chachu yaweza kuwa maziwa ya mtindi uliyonunua ya pakti, au hamira kidogo sana), then yaache bila kuyagusa/tikisa/sumbua labda kwa usiku mzima. Kesho ukiyaangalia unakuta yameshakua mtindi mzuri kabisa. Then unaweza badili chombo au kuweka katika fridge tayari kwa kuliwa.

Wengine katika kuchachua huwa waweki chochote wanayaacha yalale hivyo hivyo yataanza kuganda na kutengeneza mtindi yenyewe, sijui kwa wao lakini kwa mimi huwa naona yanatengeneza kaharufu fulani hivi kabaya. Kwahiyo njia yangu ya kuyachachua ni kuweka mtindi ule wa pakti kidogo tu kama robo kikombe. Same as hamira pia ukitumia italeta kiharufu fulani.

NB: 1. Kuwa na vyombo viwili maalumu kwaajili ya maziwa tu, kimoja gandishia, asubuhi yakishaganda hamisha kwenye chombo kingine, kile cha mwanzo osha kausha subiri routine nyingine utaanza nacho. Mzunguko unakua huo huo, isipite siku mbili bila kubadili na kuosha chombo chako.

2. Harufu husabishwa na uchafu wa chombo cha maziwa, au maziwa yalianza kugandishwa yakiwa bado ya uvuguvugu.
 
Back
Top Bottom