Uzi wa vyakula tu

Uzi wa vyakula tu

Nimetamani
Karibu, nipo nafundishwa na bimkubwa kupika biscuits zikiiva nitaleta mrejesho then kesho nitapika peke yangu. Nitajifunza na keki niwe pro kama wewe huwa unanitamanisha kweli yaani.
20230219_223521.jpg
 
Michemsho ni mizuri pia

Ila ukitaka matokeo ya haraka kula matunda tu.

Sasahivi tunaenda Kwaresma kwa Wakristo
Na Ramadhan sijui wanaanza lini.

Hivi vipindi ni vizuri sana kwa kulose weight
Jaribu uwe unafast.

Anza taratibu unafast siku 1,I unaruka
Hivyohivyo
Baadaye ukizoea unakuwa unafast mfululizo hata wiki

Tumbo na manyama uzembe yote yanapotea.
Kwaiyo nikishinda njaa mchana usiku nakula kidogo au na usiku sili pia yaani nilikuwa naomba unipe full diet routine ya jinsi ya kufanya ili angalau nikate 10kg zimenielemea jamani tusaidie tupe wewe ratiba yako madam unayotumia na inayokupa matokeo plz!
 
Mimi sipunguzi mwili maana tayari nina mwili mdogo
Ila ukitaka kupunguza mwili,funga angalau wiki moja ndani ya mwezi.

Unakula usiku tu.
Kula chakula cha kutosha.

Kama ndio mara ya Kwanza kwako kufunga,basi funga kula chakula ila maji kunywa kiasi.

Ukila usiku,ndio kesho yake usiku.

Hii njia huwa inapunguza sana mwili,Hasa tumbo,yaani tumbo linabaki flat.
 
Hamna
Ukihofia mapema kuwa utayapata na utayapata kweli.

Mimi huwa mafunga kwa ajili ya maombi,na sijawahi kuumwa vidonda vya tumbo kwa sababu ya kufunga.
Ila usiku huwa nahakikisha nimekula chakula cha kutosha na kunywa maji ya kutosha.
Wiki moja tu kilo zinakatika.
Madamu ni kweli nahitaji mateokeo ya haraka naomba nipe mwongozo wa ratoba ya kufanya nifanyeje nipe ratiba yako kwa faida ya watu wenginw ambao pia hawawezi kuuliza
 
Madamu ni kweli nahitaji mateokeo ya haraka naomba nipe mwongozo wa ratoba ya kufanya nifanyeje nipe ratiba yako kwa faida ya watu wenginw ambao pia hawawezi kuuliza
Kila wiki ya mwisho wa mwezi nakuwa na maombi ya mfungo
Kwahiyo kwa Imani yako waweza kufunga.

Kama ni mzoefu kufunga,Unakuwa unafunga kutwa nzima.. Unakula usiku tu .
Mida ya kufungua kunywa hata uji au chai ili kulainisha tumbo humo ndani,baada ya muda sasa hata saa 3 au 4 ndio Unakula chakula.
Kula chakula cha kutosha maana ni hadi kesho tena jioni.

Ukiwa huna uzoefu sana wa kufunga,basi funga kula chakula tu kutwa nzima
Ila unakuwa unakunywa maji.
Usije zima kwa njaa [emoji16].

Siku 5-7 Kila mwezi zinatosha kabisa kukufanya upunguze uzito.
 
Back
Top Bottom