Uzi wa wanaopinga Katiba Mpya

Uzi wa wanaopinga Katiba Mpya

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Wale wanaopinga katiba mpya huwa wana hoja hizi;

1. Katiba Mpya ni gharama kubwa sana. Tufafanulienei ni gharama kiasi gani?

2. Katiba mpya haitaleta pesa mfukoni au chakula mezani.

Katiba ya sasa inafanya haya mambo?

3. Katiba mpya ni ya wanasiasa wanaotaka kuingia Ikulu.
Hii katiba ya sasa ni kipingamizi kwa baadhi ya vyama kuingia Ikulu.

4. Kama watu wanalalamika hii inavunjwa hata hiyo mpya itavunjwa tu.

Hii ni hoja fikirishi na inayoibua mjadala, mnaweza kuilezea zaidi mashiko yake

5. Muda wa Katiba mpya bado.

Lini mnafikiri tutakuwa tayari kuipata hiyo Katiba Mpya

Karibuni wale mnaopinga katiba mpya mtupe ufafanuzi wenu wa hoja hizi na muongeze nyingine ambazo mnadhani ni hoja nzito za kupinga nchi kuwa na Katiba Mpya.
 
Back
Top Bottom