Uzi wama-second born

Masecond born hatuna stress....kazi kujikalia sebuleni na kusikiliza first born na last born wanavyorushiana maneno....

Huku tunajismea mioyoni heehehe...hawa hawakumbwa na corona.
 
Ukiwa second born una nafasi kubwa ya kufanikiwa. Sababu njia inakua ishatengenezwa na support kutoka kwa first born
 
Upuuzi umezidi humu, shule zimefungwa ndio shida yake, subiri umalize kula kwa kengere utajua kama kuna mtiririko wa 1st, 2nd, 3rd...9th bornie
 
Kuwa second born af first born wa kike ni changamoto sana nimepigana sana na dada angu wakati tuko wadogo na walikua wananichangia na mdogo wangu wa kike third born basi ugomvi ukianza hapo wa kuja kuamua ni mzazi pekee tena aje na fimbo nzito akichelewa tu atanikuta nimechakaa na alama za meno na kucha ila wao lazima wavimbe macho,
Aisee raha raha kuwa second born lakini second born ndo mtu anaeangaliwa Sawa na familia maana kama first born akifanya vizuri watakuangalia nawe uige kizuri alichofanya na kama first born alifanya vibaya basi utaangaliwa tu kama utafata njia zake mbovu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…