Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara

Hapa kuna 'Hunting Block' za uwindaji sijasema zifutwe. Na kwa sababu ziko eneo la chini basi eneo la juu ligeuzwe kuwa National Park na iitwe Nyerere National Park. Bwawa liitwe Bwawa la Nyerere ili vizazi vijavyo vikumbuke mambo mazuri ya Nyerere
Rais Magufuli anaonekana kumpenda mno Marehemu Nyerere maana vitu vikubwa ameviita Nyerere.
 
Hapo kwenye umeme wa jua mheshimiwa kanigusa sana, mimi huwa najiuliza inakuwaje miji na majiji yetu yanakuwa na giza wakati tungeweza kufunga taa kila kona hasa barabarani kwa kutumia solar maana jua lipo la kutosha maeneo mengi ya nchi natamani kunzisha huo mradi lakini bila government suport itakuwa ngumu kidogo. Ila kupanga nikuchagua tukifanya hivyo tunaweza kuwa na miji ya kisasa kabisa na ya mfano hapa Afrika.
 
Magufuli Majaliwa na Mama Samia Hawa waheshimiwa ni utatu uliotukuka hakika tutawakumbuka sana hawa viongozi.
 
Sorry kuuliza SI ujinga hizo pesa zilizorudishwa na Kenya ni mali ya serikali au benki ya biashara ya NBC zilikoibiwa?
 
Hivi kilo 38 ya dhahabu inaweza kuwa na value ya billion 5. Assuming 1kg ni 100,000,000tsh. 38 kg ni 3,8000,000,000
 
Hongera mheshimiwa rais na serikali yako ya awamu ya tano.

Huu mradi usipokuwa na mizengwe ya hapa na pale na kukamilika kama ulivyopangwa tutapiga hatua kubwa maendeleo sana.
 
Huku kuna hotel chumba kimoja dola elfu 3 ebu kaikagueni kama kweli kuna watanzania wanalalamo maana kwa jinsi tulivyobana mianya ya rushwa haikutakiwa iwe wazi mpaka Leo,mwisho wa kunukuu
 
Safi sana Mh. John Pombe Joseph Magufuli, endelea kufanya kazi kwa wengi maendeleo tunayaona isipokuwa huku mitandaoni wanakusema sana ila kiuhalisia wananchi wengi wanakuelewa.

Chapa kazi Mh. Rais wananchi wa Tanzania tuko pamoja nawe...
 
Umeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,

Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
 
"Ukiona umeenda kwenye pori na kuna nyuki ni wakali sana,ujue kuna ASALI".Tanzania will be great.!
 
Hivi inatumika kadri anavyoona yeye au inabidi iingie mfuko mkuu was hazina ili zipangiwe matumizi na Bunge?
Kama bwana litakuwa kivutio cha utalii, hadi sasa Mtera na Kidatu yamevutia watalii wangapi au huvutia wangapi kwa mwaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…