idawa
JF-Expert Member
- Jan 20, 2012
- 25,284
- 38,364
Kwa kuongeza tu, ule si ushahidi mahakamani.?Sorry kuuliza SI ujinga hizo pesa zilizorudishwa na Kenya ni mali ya serikali au benki ya biashara ya NBC zilikoibiwa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa kuongeza tu, ule si ushahidi mahakamani.?Sorry kuuliza SI ujinga hizo pesa zilizorudishwa na Kenya ni mali ya serikali au benki ya biashara ya NBC zilikoibiwa?
Hili swala inaonekana limemuuma sana Mheshimiwa kuwa Ndani ya Tanzania kuna hoteli Chumba milioni saba kwa siku....Huku kuna hotel chumba kimoja dola elfu 3 ebu kaikagueni kama kweli kuna watanzania wanalalamo maana kwa jinsi tulivyobana mianya ya rushwa haikutakiwa iwe wazi mpaka Leo,mwisho wa kunukuu
Nakuhakikishia huyu ni kati ya watanzania watakao andikwa na kutajwa sana miaka mingi ijayo.Ngoja aje atoke madarakani tuone kama mtaimba tena hizi nyimbo
Kupongeza juhudi ni utamaduni unaowashinda wengi, kwa hii comment yako inaonyesha ulivyo mweupe kichwani, ili uzalishe hiyo GB ni lazima uanze na MB ? Na ndicho kilichofanyika au ww ulitakajeUmeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,
Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
Leo Julai 26, 2019 Mhe. Rais Magufuli atakuwa mgeni rasmi kwenye uwekaji jiwe la msingi la mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji
Rais Magufuli aliwasili Rufiji akitokea Dar es Salaam akitumia treni ya reli ya TAZARA kwa kupitia Fuga na Kisaki
UPDATE:
Waziri wa Nishati, Medard Kalemani;
Rais ulipotuita Ikulu kutueleza ndoto yako kuhusu mradi huu, wengi hatukuelewa lakini sasa tumeanza kukuelewa. Mradi huu utatekelezwa kwa miezi 42 na mpaka sasa umeshatekelezwa kwa miezi 6
Dkt. Kalemani: Mradi huu utakapokamilika utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitatumika kuendesha treni ya umeme. Umeme huu pia utasafirishwa hadi Chalinze na baadaye Dar es Salaam na Dodoma. Tunatazamia utasaidia sana kuendesha viwanda hapo baadaye
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Kampuni hizi zinazojenga mradi huu zimefanya maajabu makubwa kule nchini Misri. Pacha wako Rais wa Misri, Fattah al-Sisi amejenga Mfereji wa Suez mwingine ndani ya kipindi kifupi. Nyie Marais nyieeee
Rais Magufuli:
Napenda nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kuwa hai siku ya leo. Napenda kumshukuru Waziri wa Nishati kwa kunialika, nawashukuru pia Mabalozi na wageni wetu kutoka Misri. Hiki ni kielelezo cha urafiki
Hapa kwetu umeme unauzwa zaidi ya senti 11, gharama za umeme zinafanya kupanda kwa bei ya bidhaa na mwisho haziwezi kushindana kwenye soko. Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa ni Taifa huru, mradi huu umepata upinzani kutoka nje na ndani
Nchi yetu ni huru na wala sio masikini, tuliamua kujenga kwa fedha zetu za ndani kupitia kodi zinazokusanywa kutoka kwa Wananchi. Fedha hizi watalipwa Waafrika wenzetu, hii ni ishara kuwa Waafrika tukiamua tunaweza
Huku kuna sehemu chumba kimoja mtu analala kwa dola 3,000. Watu wanakuja na kuondoka huku. Sijui kama Mawaziri mnajua hizo fedha tunapata asilimia ngapi, wala sijui kama vyombo vya usalama vinajua mali kiasi gani inasafirishwa kutoka hapa
Kiasi cha umeme kitakachozalishwa hapa hakijawahi kuzalishwa katika historia ya nchi yetu. Kwa sasa nchi yetu inazalisha umeme Megawati 1,601. Natarajia umeme utakaozalishwa hapa utasaidia kushusha gharama za umeme
Tanzania inaongoza kwa utunzaji wa mazingira. Maeneo tuliyoyatenga ni makubwa mno. Mradi huu utaongeza fursa katika sekta ya kilimo. Kule Mtera na Nyumba ya Mungu shughuli za uvuvi zilishamiri baada ya ujenzi wa mabwawa
Kwenye hii Selous kuna maeneo ya kuwindia (Hunting Block) 47 watu wanakuwa wanaua Simba wanaondoka na gharama kwa mwezi ni Dola 5,000. Ukilipa hiyo unaruhusiwa kuwinda hata ukiua Nyati 10. Ukweli uwindaji haulipi kwenye hii mbuga
Naomba kuanzia leo hili eneo la uwindaji likatwe, tulifanye kuwa National Park. Mataifa mengine hayafanyi sana hizi shughuli. Waziri uende ukakae kwenye Wizara mkapunguze eneo la uwindaji, hilo limesemwa sana lakini utekelezaji umechelewa
Hapa kuna 'Hunting Block' za uwindaji sijasema zifutwe. Na kwa sababu ziko eneo la chini basi eneo la juu ligeuzwe kuwa National Park na iitwe Nyerere National Park. Bwawa liitwe Bwawa la Nyerere ili vizazi vijavyo vikumbuke mambo mazuri ya Nyerere
Juzi zimerudishwa Dhahabu kutoka Kenya ambazo thamani yake ni zaidi ya bilioni 5, hizo Fedha zianze kujenga barabara kutoka Fuga kuja hapa. Tuanze kutengeneza pole pole hizi Kilomita 60. Leo watu wanaweza wasielewe
Serikali imeendelea kutekeleza miradi mingine na tunatekeleza miradi mikubwa ya kusafirisha umeme. Naipongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa miradi hii ambayo imepunguza mgao wa umeme. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni
Kutokana na TANESCO kupunguza kuagiza vifaa kama nguzo na 'transformer' kutoka nje, Viwanda 15 vimeanzishwa na kuzalisha ajira zaidi ya 3,000. Niwasisitize Wakandarasi kutekeleza mradi huu ndani ya wakati na unatarajiwa kutimia Juni 2022
Kumekuwa na mabishano kati ya NIC(Wanaotoa Bima), TANESCO na Makampuni yanayojenga hapa. Bima lazima itolewe na Serikali, ole wenu akasaini Bima na mtu mwingine. Vibali vya Wafanyakazi vitolewe mapema lakini isiwe utolewaji holela
Wananchi wa eneo hili ndio wakapewe kipaumbele cha ajira kwa sababu wao ndio wamelilinda pori hili tangu kuumbwa kwa dunia. Vyombo vya ulinzi na usalama, viuchukue mradi huu kama mboni ya nchi. Nitashangaa kama JKT hawatahusika kufanya kazi hapa
Natoa wito kwa Wizara kuanza kutekeleza kuzalisha umeme kwa njia nyingine kama jua, joto na upepo. Wananchi kama Pwagu wa kule Njombe wanaojitokeza kuzalisha umeme waungwe mkono kwani wanaweza kuzalisha umeme katika vijiji vyao
Ndugu zangu Wananchi namalizia na maneno haya, 'Ukiona umeenda kwenye pori na nyuki ni wakali sana ujue kuna asali'. Hapa kuna asali ndio maana watu walipiga kelele. Ukiamua kufanya mradi wako fanya usisubiri watu wakushauri
Huku kuna hoteli kubwa kuliko hoteli za Dar es Salaam. Chumba kimoja dola 3,000 na ina vyumba 15. Sijui kama Serikali inapata mapato. Muda wa kuchangamka ni sasa. Wizara ya Maliasili kagueni hiyo hoteli mjue Serikali inaingiza kiasi gani
Kwani Nyerere alihamisha mbuga ya wanyama kama jiwe? we bashite kweliRais Magufuli anaonekana kumpenda mno Marehemu Nyerere maana vitu vikubwa ameviita Nyerere.
Una utaalam wowote wa Mambo ya umeme?Umeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,
Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
We we halijakuuma mkuu,yaani milioni 7 halafu bado usingizi hakunaHili swala inaonekana limemuuma sana Mheshimiwa kuwa Ndani ya Tanzania kuna hoteli Chumba milioni saba kwa siku....
Unajua utofauti wa hili bwawa na uliyoyataja? Muwe na akili za kujiongeza basi.Hivi inatumika kadri anavyoona yeye au inabidi iingie mfuko mkuu was hazina ili zipangiwe matumizi na Bunge?
Kama bwana litakuwa kivutio cha utalii, hadi sasa Mtera na Kidatu yamevutia watalii wangapi au huvutia wangapi kwa mwaka?
Bwawa kuwa tourist attraction. Kwa mfano lipi la nchi gani?Unajua utofauti wa hili bwawa na uliyoyataja? Muwe na akili za kujiongeza basi.
Hapa kuna 'Hunting Block' za uwindaji sijasema zifutwe. Na kwa sababu ziko eneo la chini basi eneo la juu ligeuzwe kuwa National Park na iitwe Nyerere National Park. Bwawa liitwe Bwawa la Nyerere ili vizazi vijavyo vikumbuke mambo mazuri ya Nyerere
Juzi zimerudishwa Dhahabu kutoka Kenya ambazo thamani yake ni zaidi ya bilioni 5, hizo Fedha zianze kujenga barabara kutoka Fuga kuja hapa. Tuanze kutengeneza pole pole hizi Kilomita 60. Leo watu wanaweza wasielewe
Chene anguHapa maendeleo tu. Hakuna longolongo. Pongezi nyingi kwa Igembe Lise JPM.
Si unajua masikini tulivyoHili swala inaonekana limemuuma sana Mheshimiwa kuwa Ndani ya Tanzania kuna hoteli Chumba milioni saba kwa siku....
Achana na Nyerere haki ya Mungu Kuna vitu nikiandika humu viwili tu kuwa kwa Nini Nyerere alitaka makao makuu yawe Dodoma yahame toka Dar es salaam mama Maria Nyerere ataniunga mkono na kutukana matusi ya nguoni kutukana Marehemu Nyerere.Kwa Nini Nyerere alihamisha makao makuu kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma kamuulizeni Mama Maria Nyerere.Nina hasira hapa nilipo .Mama Maria Nyerere usiogope waambie.Dodoma Kuna tetemeko la Ardhi Dodoma Kuna uranium inatema mionzi inaathiri mimba watu vipofu wanazaliwa kibao.Nchi ijiandae kuzalisha vipofu kibao kwa mimba zitakazotungwa Dodoma kwa mimba kupigwa na miale ya Uranium madini yanayotumika kuzalisha mabomu ya nuklia.Kama makabila mengine mlikuwa mnacheka wagogo kuwa na vipofu wengi jiandaeni kuwa na vipofu wengi wasio wagogo.Uranium inatema mionzi hewani Dodoma masaa 24 kuathiri mimba.Kilichopelekea Nyerere apeleke makao makuu Dodoma Mama Maria Nyerere anakijua vizuri Sana sikianiki Maria Nyerere Mwenyewe ajibu.Raisi Magufuli Kuna vitu asione wajinga maraisi waluomtangulia waliogoma Kuhamia Dodoma Siri anayo Maria NyerereKwani Nyerere alihamisha mbuga ya wanyama kama jiwe? we bashite kweli
Acha kutunga uongoNchi ijiandae kuzalisha vipofu kibao kwa mimba zitakazotungwa Dodoma kwa mimba kupigwa na miale ya Uranium madini yanayotumika kuzalisha mabomu ya nuklia
Raisi Magufuli Kuna vitu asione wajinga maraisi waluomtangulia waliogoma Kuhamia Dodoma Siri anayo Maria Nyerere
Hii kali! yaani hiyo siri Rais wa nchi haifahamu ila unaifahamu wewe na Mama Maria Nyerere, huu uongo huwa mnafundishwa wapi?Kuna vitu nikiandika humu viwili tu kuwa kwa Nini Nyerere alitaka makao makuu yawe Dodoma yahame toka Dar es salaam mama Maria Nyerere ataniunga mkono na kutukana matusi ya nguoni kutukana Marehemu Nyerere.