Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara

Sorry kuuliza SI ujinga hizo pesa zilizorudishwa na Kenya ni mali ya serikali au benki ya biashara ya NBC zilikoibiwa?
Kwa kuongeza tu, ule si ushahidi mahakamani.?
 
Huku kuna hotel chumba kimoja dola elfu 3 ebu kaikagueni kama kweli kuna watanzania wanalalamo maana kwa jinsi tulivyobana mianya ya rushwa haikutakiwa iwe wazi mpaka Leo,mwisho wa kunukuu
Hili swala inaonekana limemuuma sana Mheshimiwa kuwa Ndani ya Tanzania kuna hoteli Chumba milioni saba kwa siku....
 
Ngoja aje atoke madarakani tuone kama mtaimba tena hizi nyimbo
Nakuhakikishia huyu ni kati ya watanzania watakao andikwa na kutajwa sana miaka mingi ijayo.

Ataacha alama nyingi sana zile za vitu vinavyoshikika na vile vya kifalsafa/itikadi.

Asipotajwa kwa mema atatajwa kwa aliyo shindwa kufanya vizuri.
 
Umeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,

Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
Kupongeza juhudi ni utamaduni unaowashinda wengi, kwa hii comment yako inaonyesha ulivyo mweupe kichwani, ili uzalishe hiyo GB ni lazima uanze na MB ? Na ndicho kilichofanyika au ww ulitakaje
 
Hilo la vyumba vya hoteli na mimi niliwahi kujiuliza sana. Mfano kule Mafia kuna mwekezaji amepewa kakisiwa, gharama zake sasa. Hadi jina la kisiwa limebadilishwa. Serikali ina utarabitu gani kupata mapato stahiki kwenye mahoteli?
 
Dhana kuwa ukimlipa mwafrika unakuwa umekwepa mabeberu siyo sahihi.

Hiyo kampuni ya Misri ina mikopo na mikataba mikubwa na kampuni na taasisi za fedha nje ya Afrika. Unapofanya kazi naye, indirectly unakuwa unafanya na watu hao.

Ukifanya kazi na mtu kama Dangote, ni hivyo hivyo. Sasa sana gharama za mikopo na miradi zinaongezeka kulinganisha na kama wewe ungewatafuta hao mabeberu moja kwa moja.

Nadhani Magufuli halijui hili. Inabidi aelimishwe.
 
Hata ile Gesi ya Mtwara mliifungua kwa mbwembwe nyingi, wafanyabiashara wakaenda kujenga mahotel lkn sasahivi wanalia. miradi inayoanzishwa bila kuwa na business plan ni sawasawa na kilimo cha mvua, then jua lije liharibu kila kitu. Watanzania kamwe hatutatoka na hizi sinema.
 
Umeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,

Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
Una utaalam wowote wa Mambo ya umeme?
Haters are siblings of Satan!
 
Hivi inatumika kadri anavyoona yeye au inabidi iingie mfuko mkuu was hazina ili zipangiwe matumizi na Bunge?
Kama bwana litakuwa kivutio cha utalii, hadi sasa Mtera na Kidatu yamevutia watalii wangapi au huvutia wangapi kwa mwaka?
Unajua utofauti wa hili bwawa na uliyoyataja? Muwe na akili za kujiongeza basi.
 
Nitampinga kwa vingine vyote ila sio swala linalohusu umeme nasimamia ninacho kiamini.
 
Hongera Mh.Rais JPM na team yako mzima,sisi Watanzania tunaendelea kuwaombea katika ujenzi wa nchi kwa vitendo.
Asiyekushukuru achana naye kwani asiyefanya hivyo hata wanyama na mimea watawashukuru.
 
Hapa nimekuelewa ipasavyo...
 
Kwani Nyerere alihamisha mbuga ya wanyama kama jiwe? we bashite kweli
Achana na Nyerere haki ya Mungu Kuna vitu nikiandika humu viwili tu kuwa kwa Nini Nyerere alitaka makao makuu yawe Dodoma yahame toka Dar es salaam mama Maria Nyerere ataniunga mkono na kutukana matusi ya nguoni kutukana Marehemu Nyerere.Kwa Nini Nyerere alihamisha makao makuu kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma kamuulizeni Mama Maria Nyerere.Nina hasira hapa nilipo .Mama Maria Nyerere usiogope waambie.Dodoma Kuna tetemeko la Ardhi Dodoma Kuna uranium inatema mionzi inaathiri mimba watu vipofu wanazaliwa kibao.Nchi ijiandae kuzalisha vipofu kibao kwa mimba zitakazotungwa Dodoma kwa mimba kupigwa na miale ya Uranium madini yanayotumika kuzalisha mabomu ya nuklia.Kama makabila mengine mlikuwa mnacheka wagogo kuwa na vipofu wengi jiandaeni kuwa na vipofu wengi wasio wagogo.Uranium inatema mionzi hewani Dodoma masaa 24 kuathiri mimba.Kilichopelekea Nyerere apeleke makao makuu Dodoma Mama Maria Nyerere anakijua vizuri Sana sikianiki Maria Nyerere Mwenyewe ajibu.Raisi Magufuli Kuna vitu asione wajinga maraisi waluomtangulia waliogoma Kuhamia Dodoma Siri anayo Maria Nyerere
 
Nchi ijiandae kuzalisha vipofu kibao kwa mimba zitakazotungwa Dodoma kwa mimba kupigwa na miale ya Uranium madini yanayotumika kuzalisha mabomu ya nuklia
Acha kutunga uongo
Raisi Magufuli Kuna vitu asione wajinga maraisi waluomtangulia waliogoma Kuhamia Dodoma Siri anayo Maria Nyerere
Kuna vitu nikiandika humu viwili tu kuwa kwa Nini Nyerere alitaka makao makuu yawe Dodoma yahame toka Dar es salaam mama Maria Nyerere ataniunga mkono na kutukana matusi ya nguoni kutukana Marehemu Nyerere.
Hii kali! yaani hiyo siri Rais wa nchi haifahamu ila unaifahamu wewe na Mama Maria Nyerere, huu uongo huwa mnafundishwa wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…