Uzinduzi Mradi wa Umeme, mto Rufiji: Rais Magufuli aagiza sehemu ya Selous kuwa Hifadhi ya Taifa. Fedha zilizorudishwa kutoka Kenya kujenga barabara

Mwalimu Kichuguu unaifahamu vizuri jiografia ya nyanda za juu kusini na vyanzo vya maji ya mto rufiji?
Sijui sawasawa lakini technologia ya hyropower inategemea sana kiasi cha maji yanayopita pale. Kama turbine hizo zinahitaji maji ya kiasi cha mita za ukubwa 10000 (kwa mfano tu) ambazo ni nyingi kuliko zile za Kidatu ambazo ni mita 2000 (kwa mfano tu), na kwa sasa zinapatikana Rujifi. Iwapo hali ya hewa ikabadilika mto rufiji ukabaki na meta za ukubwa 8000 ambazo bado ni nyingi sana kuliko za kidatu, zile turbines zake hazitafanya kazi.

Sijui umeelewa mfano wangu huo. kwa hiyo tatizo siyi wingi wa maji tu, bali pia kutosheleza mahitaji ya turbines zilizosimikwa pale
 
Naelewa wasi wasi wako kuhusu kina cha maji ya kutosha kwa mwaka mzima ili kuwa na msukumo sahihi wa kuendesha mitambo (pressure in fluid increases with depth). Kwa maneno mengine, wasiwasi wako ni kujua kama kwa wastani kiasi cha maji yanayoingia bwawani yanakaribia kuzidi yale yanayotoka ili kina sahihi cha bwawa kiwepo wakati wote.

Nikutoe wasiwasi...

Tofauti kati ya bwawa la Kidatu (blue circle on the map) na Rufiji ni kwamba hii Stiegler's Gorge (red circle on the map) ipo kwenye kiungio cha mito mitatu ikiwemo Ruaha unaojaza Kidatu. Mito mingine ni pamoja na Kilombero (Ulanga) na Luwego, hivyo kukosekana kwa maji ya kujaza bwawa siyo tatizo kwakuwa vyanzo vyake vinatoka sehemu tofauti.

Eneo lote hilo la vyanzo vya mito hiyo mitatu inauoto wa asili wa kutosha ambao ni kiashiria cha uwepo wa maji mengi. Uoto wa asili mwingi kutengeneza mvuke unaoleta mvua. Pia eneo la mraba lililoinuka nyanda za juu kusini (elevation. 1700m) ni kubwa sana kiasi cha kuweza kukusanya maji mengi (upstream) na kuyamwaga (downtream) huko kwenye Stiegler's Gorge na kuhakikisha kuna mtiririko wa maji mwaka mzima.

Screenshot_2019-07-27 File Rufiji River basin map svg - Wikipedia.png
 
View attachment 1165161
Hii hukujibu wasiwasi wangu. Swali ni kjuhusu uwiano kati ya kina cha maji na mitambo inayoendeshwa na maji hayo.
 
Umeme wenyewe ni megawatts(MB)2000, yan ungefikia kwenye hata Gigawatts(GB) 1 sijui ingekuwaje hayo makelele yake,

Nathan serikali ianze kufikiria kuzalisha gigawatts za umeme
1) a man brags his penis however tiny.
2) a boy driving his father's expensive car has no say in front of men riding their own bicycles.
3) one bird in hand wealths hundreds in air
4) Rome was not built in a single day
 
Hii hukujibu wasiwasi wangu. Swali ni kjuhusu uwiano kati ya kina cha maji na mitambo inayoendeshwa na maji hayo.
Hilo ni suala la designing ya bwawa, watakuwa wamelizingatia. Hawawezi tuu kuwa wamejichagulia turbines bila kukokotoa kiasi cha ujazo wa maji yatakayo hifadhiwa bwawani.
 
Sijui sawasawa lakini technologia ya hyropower inategemea sana kiasi cha maji yanayopita pale. Kama turbine hizo zinahitaji maji ya kiasi cha mita za ukubwa 10000 (kwa mfano tu) ambazo ni nyingi kuliko zile za Kidatu ambazo ni mita 2000 (kwa mfano tu), na kwa sasa zinapatikana Rujifi. Iwapo hali ya hewa ikabadilika mto rufiji ukabaki na meta za ukubwa 8000 ambazo bado ni nyingi sana kuliko za kidatu, zile turbines zake hazitafanya kazi.

Sijui umeelewa mfano wangu huo. kwa hiyo tatizo siyi wingi wa maji tu, bali pia kutosheleza mahitaji ya turbines zilizosimikwa pale

Hiyo ni tech ya zamani. Kuna system inayo regulate kiasi cha maji kinacho hitajika kulingana na mahitaji ya umeme. Maana siyo wakati wote umeme utakaohitajika ni mg 2000+ kuna high and low season.
Pia siyo kwamba kutakuwa na mtambo mmoja utakaozalisha mg 2000. Bali ni number of turbines. Hivyo maji yakipungua kuna turbines zitakuwa zinafungwa.
 
Kuwepo kwa spillway ni kitu kimoja, lakini kiasi cha KE inyohitajika kuendesha turbine fulani ni kitu kinginee kabisa; ukizima turbine moja haina maana kuwa KE energy iliyotakiwa kuangukia kwenye trubine hiyo itaangukia kwenye trubine nyingine. Ni iwapo plant imejengwa kwa target ya MW2100 halafu baadaye inakuwa regulated ku-generate kiasi kidogo kwa sababu nilizozungumzia ambazo haziko kwenye control yetu italazimisha power generation iwe chini ya capacity hiyo. Na kumbuka mazowea yana tabu; tutalalamika tena kuwa umeme hautoshi
 
Screenshot_20190728-181644_Chrome~2.jpeg
FB_IMG_1564293604841.jpeg
Hivi Issue ya EIA (Environmental Impact Assessment) Ya Hii Project Iliishiaga Wapi?
 
Attachments

  • Screenshot_20190728-181644_Chrome~2.jpeg
    Screenshot_20190728-181644_Chrome~2.jpeg
    38.6 KB · Views: 13
Mambo makubwa mawili yaliyofanywa na Rais Magufuli juzi Julai 26, 2019 ni ya kupigiwa mfano na Watanzania wote hatuna budi kumshukuru Magufuli kwa maamuzi yale magumu.

Nazungumzia kuanza ujenzi wa mradi wa umeme wa mto Rufiji ambao ulibatizwa na Wazungu kwa jina la Stieglers’ Gorge Power Project na kumegwa kwa pori la akiba la Selous na kuanzisha Hifadhi Mpya ya Taifa itakayoitwa Nyerere National Park ama kwa jina la kimombo Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Asante sana JPM.

Labda kabla ya kueleza kwa nini Watanzania hatuna budi kushukuru tuwekane sawa kuhusu iliyoitwa Stieglers’ Gorge na Selous Game Reserve.

Jina Stieglers ni la Mswisi ambaye alikuwa Engineer. Alikwenda Selous, hapo kwenye gorge, kufanya utafiti wa kujenga bwawa la kufua umeme na Daraja. Akiwa hapo akauawa na tembo, na mahali hapo pakapewa jina la Stieglers’ Gorge mwaka huo 1907. Kabla ya tukio hili palikuwa panaitwa Pangani Rapids.

Kuhusu jina la Selous. Huyu alikuwa ni Mjerumani, ambaye alikuwa ni mwindaji na mwandishi wa habari. Huo ni wakati Tanzania ikiwa chini ya utawala wa Mjerumani. Eneo hilo lilikuwa linaitwa Field of Lady (_yaani Shamba la Bibi_) na wenyeji wengine waliliita Kitaluni. Vita ya Kwanza ya Dunia ilipoanza, yeye Bw. Selous alikuwa huko. Akaingizwa kupigana akiwa hukohuko, na akafariki 1917. Baada ya hapo eneo likaitwa Selous.

Kwa hiyo wale walioanza kupitisha maneno ya kulaumu na kutoa lugha mbovu juu ya hatua ya Rais Magufuli kubadili majina haya watambue kuwa majina hayo ni ya wakoloni na kuyaendeleza maana yake ni kuwaenzi wakoloni waliotunyonya na kuwanyanyasa mababu zetu kwa miaka nenda rudi.

Narudia Watanzania hatuna budi kumshukuru JPM kwa maono yake na kutuzindua usingizini kwa sababu hakuna aliyekuwa akiwaza ama kupendekeza juu ya rasilimali hizi kubwa ndani ya Taifa letu kupatiwa majina ya nyumbani badala ya kubaki na majina ya wageni.

Tukiachana na hilo, JPM ametufumbua macho kwa jambo jingine kubwa kwamba wakati tukipumbazwa kwa majina haya ya wageni na kufunikwa kwa makoti ya kuhifadhi mazingira tunapaswa kutumia rasilimali hizi kwa manufaa yetu.

Ni bahati mbaya sana hakuna aliyewahi kudadisi jambo hili.

Tulikaa kimya wakati tunaambiwa tusijenge mradi wa kuzalisha umeme katika mto Rufiji eti tutaharibu mazingira wakati hao wanatuambia tusijenge mradi huu kampuni zao na watu wao wamejenga mahoteli ndani ya Pori la Selous, wanakuja kupumzika na kuwinda wanyama wetu katika vitalu 47 vya uwindaji, wanataka kuchimba madini ya uranium, wanafanya tafiti zinazohusisha shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi na wametengeneza viwanja vya ndege 38 ambavyo ndege zinatua na kuruka pasipo uwepo wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vyenye dhamana ya kujua nini kinatoka na nini kinaingia.

Tukubali tu hapa napo tumepigwa sana, tena sana tu. Asante JPM.

Tulikaa kimya wakati tulipoambiwa Selous Game Reserve ni moja ya maeneo ya urithi wa dunia (world heritage sites) tukashangilia sana sana na kujinasibu kwa kila aina ya majigambo. Kwa bahati mbaya sana tukasahau kuwa kuingia katika mtego huo tunapoteza zaidi.

Selous inapokuwa Game Reserve maana yake hapa ndio panakuwa paradiso ya hao jamaa kuja kuua wanyama wetu na kustarehe ndani ya hifadhi yetu hii kubwa.

Kwa msiojua ndani ya Selous Game Reserve kuna vitalu vya uwindaji 47 vyenye hoteli za kitalii. Hoteli hizi zimejengwa mahususi kwa watalii wa kutoka nje ya nchi ambao hata malipo yao wanayafanyia nje ya nchi. Sina hakika kama mamlaka zetu za Tanzania hukusanya kodi inavyostahili katika hali hii. Ukipita hoteli zote zilizopo katika mapori ya akiba utakuta wateja wake ni wazungu tu. Ukiwauliza wafanyakazi watakwambia hatujawahi kuona Mtanzania anakuja kulala huku. Wageni wanaokwenda huko hawajawahi kuonekana wakifanya malipo. Maana yake ni kwamba wanalipia wakiwa nje ya nchi na fedha zote zinaingia katika mataifa hayo. Hapa napo tumepigwa na tunapigwa sana. Asante JPM kwa kutufumbua macho.

Wakati tunajiuliza juu ya mapato yatokanayo na mahoteli haya makubwa ya kitalii yenye gharama ya chumba ya zaidi ya shilingi Milioni 1.5 kwa usiku mmoja pia tujiulize hawa jamaa wanaona mradi wa umeme wa Stieglers’ Gorge tu ndio mbaya kwa mazingira lakini uwekezaji wao huu wa mahoteli makubwa yaliyopo ndani ya mapori na jirani na vyanzo vya maji ikiwa ni ndani ya mita 60 ambazo sheria inakataza ni sawa?

Za kuambiwa changanya na za kwako. Asante sana JPM.

Tunamshukuru JPM kwa kuamua kutekeleza mradi wa umeme wa mto Rufiji ambao utaingiza megawati 2,115 za uneme katika gridi ya Taifa ikilinganishwa na umeme ulipo sasa ambao ni megawati 1,600 tu. Tunashukuru kwa sababu sasa safari ya ajenda ya Tanzania ya viwanda itawezekana.

Tunamshukuru pia Rais Magufuli kwa kuwa amemkumbuka Baba wa Taifa kwa kuamua kumega Pori la Akiba la Selous na kuanzisha Hifadhi ya Taifa ya Nyerere. Hii itakuwa hatua muhimu ya kuachana na jina la Selous, kuachana na kumuenzi huyu mgeni ambaye kwa miaka mingi ameenziwa pasipo kuwa na sababu ya msingi ya kubeba jina la rasilimali yetu ilihali sisi tupo.

Tutaita Hifadhi ya Nyerere na tutamuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Safi sana JPM.

Kwa wasiojua, hifadhi inapokuwa Pori la Akiba inaruhusu uwindaji na kunakuwa na juhudi ndogo za uhifadhi. Lakini inapokuwa Hifadhi ya Taifa maana yake kunakuwa na juhudi kubwa zaidi za uhifadhi kama ambavyo inafanyika Serengeti, Manyara na Mikumi.

Ukiangalia takwimu za ukubwa wa hifadhi za taifa utaona Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ina kilomita za mraba 20,226, Serengeti ina kilomita za mraba 14,763 na Burigi-Chato ni ya tatu na ina kilomita za mraba 4,702.

Pori la Akiba la Selou ambapo linapendekezwa kuwa Hifadhi ya Taifa lina kilometa za mraba 52,000. Maana yake ni kwamba hii ndio itakuwa hifadhi kubwa kuliko zote hapa Tanzania.

Hakika inastahili kupewa jina la Baba wa Taifa. Asante sana JPM.

Hata kama itapunguzwa eneo la lenye vitalu vya uwindaji bado itabaki kuwa hifadhi kubwa kuliko zote.

Kwa kuwa Hifadhi ya Taifa, nchi yetu itapata mapato mengi zaidi ya utalii na wanyama wetu wataongezeka kwa sababu uhifadhi utaimarishwa zaidi. Tofauti na sasa ambapo wageni wamekuwa wakienda huko kujiburudisha kwa kuua wanyama wetu na kupiga nao picha. Aibu hii.

Vijana wetu wengi watapata ajira. Kwa hivi sasa Selous haizalishi ajira nyingi kwa sababu vijana wanaotegemea kupeleka wageni hawapiti fursa hiyo. Jamaa wanaokwenda kuua wanyama na kula starehe katika camp site wanahitaji askari wanyama pori tu.

Halikadhalika kwa kuwa Hifadhi ya Taifa tunaamini sasa hata maeneo ambayo waliona pori hili la Selous ni kero sasa wataanza kuona faida, watapa watalii wengi na biashara na maisha ya watu yatachangamka kama ilivyo katika maeneo mengine yenye hifadhi za Taifa kama vile Arusha, Kilimanjaro, Iringa, Morogoro na Manyara.

Lakini pamoja na kwamba tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuingilia kati masuala haya bado kuna maswali yanaumiza na kukwaza.

Hivi mpaka Rais Magufuli anasema haya, Wizara ya Maliasili na Utalii wapo na wana wataalamu, bodi za Hifadhi, Bodi ya Utalii na viongozi wake. Walikuwa wapi kufikiria mambo haya na kuyatengenezea ajenda na msukumo wa kutosha? Jitafakarini?

Hivi mpaka Rais Magufuli anaingilia kati viongozi katika ngazi za mikoa ambako miradi ipo mlikuwa wapi? Mnasubiri siku ya uzinduzi ndipo mpige mwembwe za kutueleza manufaa ya mradi? Mbona hatukuwasikia kabla? Mlipatwa na nini?

Sitaki nizisemee awamu zilizopita lakini najiuliza sana, wapo wadau wengi wanaojinasibu kuwa ni Watanzania na wanapigania maslahi ya Watanzania, hivi walikuwa hawayaoni haya?

Rais Magufuli amemuuliza Waziri wa Maliasili na Naibu wake kama hawa wamewahi kulala hoteli iliyopo mto Rufiji iitwayo Serena Mivumo na wakamjibu hawajawahi kulala. Sisi sisi wananchi tupate picha gani, kwamba hawajui hata kinachoendelea huko kwenye hizo hoteli. Hii ni aibu kubwa.

Mimi sio Boss wenu lakini Dk Kigwangallah na Mhe. Kanyasu nendeni mkakagua hoteli zote zilizopo kwenye hifadhi ili muwe na taarifa za kutosha.

Vyombo vya ulinzi na usalama, nanyi mliulizwa na hamkujibu na Mhe. Rais akasema bayana hana hakika kama mnafahamu kinachoendelea katika hoteli hizo. Kwa hakika mnapaswa kujitafakari na kuchukua hatua. Tusipojiangalia watu wanaweza kuwa wanaruka Ulaya na wanatua moja kwa moja katika mapori yetu bila vyombo vyetu kujua na wala mamlaka zetu kukusanya mapato yanayostahili.

Muhimu hapa, tumefumbuliwa macho tuchangamke. Tuachane na wachache ambao wamenunuliwa kupinga kila aina ya juhudi za kutetea maslahi ya Watanzania. Tukiwajua tuwapuuze.

Kila la kheri Watanzania. Asante sana JPM

Mzee Abdallah Makata
Morogoro.
28 Julai, 2019.w
 
Asante kwa uchambuzi wa kina .mungu akubariki sana kwa kutoa elimu kubwa
 
Game reseves zote nchini mwetu zingetambulika kama hifadhi rasmi kabisa.
 
Hakika kabisa kwa hili JPM atabaki kuwa wa pekee kwa kweli. Kuna kitu haujakigusia kaka mi naona hata usalama wa taifa unakuwa shakani maana kama watu wanaingia kimyakimya na kuondoka kimyakimya sijui hapo usalama wa nchi inakuwaje??!! Ni hatari sana. Hongera sana JPM.

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mada kubwa na fikirishi.

Ombi langu kwa wenye dhamana wawe makini wasivuruge na kuuwa biashara ya hizo hotel bali wazikumbatie na kutafuta suluhu ya kupata mapato tunayo stahili.
 
Back
Top Bottom