Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Uzinduzi rasmi wa JF Aprili 2010

Status
Not open for further replies.

Invisible

JF Admin
Joined
Feb 26, 2006
Posts
16,286
Reaction score
8,380
Heshima zenu wakuu,

Baada ya kwikwi za hapa na pale (marekebisho ya nguvu), leo tumehitimisha kabisa sehemu ambazo tunaamini zilihitaji marekebisho ya nguvu (kwenye server). Tunasikitika kwa usumbufu uliojitokeza na kuwashukuru kwa uvumilivu wenu! Tunaamini kuna utofauti mtaugundua na mtaendelea kutupa ushirikiano huku tunakoelekea.

Tunatarajia rasmi kuizindua JF mpya mwezi Aprili, 2010 ikiwa na sura mpya na vitu vipya.

JF haijajitangaza na mlio wengi mmeifahamu kwa kuambizana aidha kwa njia ya barua pepe au kwa njia ya ku-search vitu kadhaa mtandaoni na mkajikuta mnaangukia humu, wengine mkachukua hatua ya kujisajili na kuwa wanachama kabisa. Tunawashukuru kwa uamuzi wenu wa busara na wa kiungwana.

Mpaka naandika hapa, tumefikia karibia asilimia 80 ya sura mpya ya JF. Tunaandaa pia version ya JF kwa wanaotumia simu za mikononi ili iweze kuwa ina-load kwa haraka kama inavyotokea kwa wanaotumia kompyuta.

Aidha, tumepokea maoni kadhaa na yafuatayo yametiliwa maanani kwenye JF mpya ijayo:

  1. JF ni ngumu kutumiwa, wengi wanashindwa kuelewa namna ya kutuma posts na namna ya kuanzisha topic/threads na wengine hata hawajui maana ya PM na baadhi ya maneno/vifupisho vitumikavyo JF. Wengine wanatamani kuichangia JF ili iweze kufanya vema zaidi lakini hawajui wafanyeje
    • Hili tumnekuwa tukijaribu kuwaelewesha wengi lakini imeonekana ni ngumu kwa version tuliyo nayo kuweza kueleweka. Ukisoma topic hii JamiiForums - How To inaeleza wazi namna ya kuitumia JF kirahisi na pengine majibu ya maswali haya yamewekwa. Katika version mpya ijayo tumejitahidi kurekebisha na kufanya mambo mengi yawe rahisi kwa mtu anayeitembelea JF kujifunza bila kuuliza sana. Bado tunasisitiza kwa wale ambao hawajui namna ya kufanya mambo kadhaa kuuliza kwa kutuma barua pepe (email) kwenda support@jamiiforums.com nasi tutawajibu ndani ya dakika 60 tangu barua pepe imepokelewa.
    • Ukiangalia kwenye topic hii utagundua kuwa maelezo yako wazi. Tunawashukuru wanachama ambao wamekuwa wakituchangia tangu 2009 mpaka sasa na kuwaomba waendelee kutupa ushirikiano tunakoelekea sasa. Katika version mpya tumeandaa njia rahisi ambayo itampa mhusika urahisi wa kutambua anawezaje kuwa Premium Member, anawezaje kuichangia JF na hata kufafanua juu ya ranking za JF zinavyokwenda.
  2. Matusi/pumba vimezidi JF, wahusika wachukuliwe hatua!
    • Hali hii tumeshaibaini, kutokana na kugubikwa na majukumu ya kuja na kitu cha maana zaidi tunajikuta tunashindwa kutekeleza kila kitu kama ambavyo tungependa kiwe. Lakini tunapenda kuwahakikishia kuwa hali itarejea kuwa sawa mwezi April na tutahakikisha tunasafisha jamvi na kuwafahamisha wote ambao watakuwa walienda visivyo juu ya makosa yao, tunasikitika hatutafungia mtu kwa makosa yaliyopita. Tunapenda kusisitiza wana JF kuzingatia Sheria na Kanuni za JF, tunakoelekea hatutawavumilia wachafuzi wa aina yoyote.
  3. Posts/Threads zinahamishwa bila kutoa taarifa:
    • Suala hili tumekuwa tukipata taarifa zake, tunafahamu inavyokera endapo mtu anaanzisha hoja anakuja kesho yake anakuta haipo na hajapewa maelezo. Baada ya Aprili mwaka huu, tutahakikisha kila hoja inayoondolewa mhusika (aloandika) anafahamishwa kwanini hoja yake imeondolewa na kuelezwa hoja ilipohamishiwa. Kila topic inapohamishwa huachwa redirection, kwa kipindi hiki tunaomba tuwieni radhi tukamilishe ngwe ya mwisho kisha tutafuata ambacho nimeeleza hapo juu.
    • JF moderation inazidi kuwa ngumu, JF inapata hits zaidi ya milioni 45 kwa mwezi na kila siku posts zaidi ya 1,200 zinatumwa. Tumefikiria kuongeza moderator mmoja na tutaendesha semina kwa moderators wote kuweza kukabiliana na hali halisi.
  4. Nataka kutangaza JF lakini sijui nifanyeje:
    • Katika toleo la JF lijalo tumeonelea ni vema kuweka gharama za matangazo katika JF pamoja na aina za matangazo na sehemu za kutangaza ndani ya JF. Tutaweka wazi gharama bila kificho ili kila anayetaka kutangaza biashara yake kupitia kwetu aamue ni eneo gani angependa kutangaza na kivipi.
    • Tunawashukuru Zain kwa kuwa wadau wa kwanza kuchukua fursa ya kutangaza kwenye Front Page, tunaamini baada ya uzinduzi wengi wataelewa gharama zikoje na wapi pa kuwasiliana nasi ili kuweza kuweka matangazo hapa JF
    • JF yenyewe itaanza kujitangaza kuanzia Aprili 2010.
  5. Harakisheni chat hapa JF!
    • Suala hili tumelifikiria kwa upana, linafanyiwa kazi lakini namna ya chat itakavyokuwa itakuwa na utofauti kidogo na wengi wanavyotarajia, bado itakuwa userfriendly lakini itakuwa ni baina ya mwanachama na mwanachama; wasiojisajili hawataweza.
  6. Nataka kuwa na blog yangu ndani ya JF
    • Tumelifikiria hili na linafanyiwa kazi kwenye JF mpya ijayo, aidha wale wenye blogs via blogspot na wordpress tunaweza kushirikiana nao katika kuzihamishia kwenye server yetu.
  7. JF Tv/Radio/News paper
    • Kimoja au viwili vya vitajwa hapo ki(vi)taanza karibuni, tunategemea ushirikiano kutoka kwenu!
  8. Kutakuwa na 24/7 Live support ambayo itakuwa na wasaidizi watano tofauti.
Aidha, kutakuwa na sehemu ya masoko (Market Place) na kwa wale mnaohitaji email via JF msisite kuwasiliana nasi via support@jamiiforums.com ili tuwatengenezee accounts zenu. Kwa wale waliosahau password zao na wana uhakika wamewahi kujisajili, pia wawasiliane nasi kwa anuani hiyo ili tuwakumbushie majina yao na password zao.

Logo ya JF itabadilika, mwonekano kwa ujumla! Kwa wale wenye kutaka kuchukua kumbukumbu za JF hii ya sasa mnaweza kuchukua screenshot ili siku za usoni mjikumbushe kabla ya mabadiliko tunayoyafanya JF ya sasa (up to April 2010) ilikuwa ina sura gani.

Kwa niaba ya wenzangu (wawili, mimi wa tatu) napenda kuwashukuru wote mliotuunga mkono tangu tunaanza na mnaoendelea kutuunga mkono tunakoelekea. Tunaamini katika ushirikiano mengi yanawezekana!

Tunakaribisha maoni, mapendekezo na ushauri wa nini kifanyike zaidi...
 
all the best ................ i can see.......... you have something to do, please do it here..................
 
Invisible na team yako, mbarikiwe sana. Inafurahisha sana kuona JF inasonga mbele.
 
asante sana uongozi wa jf.

pendekezo langu kwa vile April ndio uzinduzi rasmi unafanyika,mnaonaje mwezi mzima wa April tutembeze harambee ya changia JF kwa chochote kile mtu alichokuwa nacho wanachama wote kwa ujumla na wageni ? Harambee hiwe inakumbushwa kila siku mpaka mwezi utakapomalizika.

ni wazo tu kama itawezekani na najua hipo thread ya kuchangia lakini kampeni kama hizi huwa zinasaidia mda mwingine huku tukiwa tunaendelea na michango ya kawaida.
 
asante mkuu...natumaini pia mtaweka sehemu ya kuingia kwenye mails moja kwa moja
 
Kikwetu tunasema, kilililiiiiiiiiiiiiiii ai ai!!!!; also known as ululation
 
Thank you very much mkuu,tutaendelea kushirikiana kuiboresha JF zaidi.,ubarikiwe sana wewe na moderators wenzako.
 
Mkuu hapa tutawasiliana ngoja chakula kitulie tumboni.
 
Hongereni sana wakuu na nawapongeza kwa hatua hii nzuri na muhimu mliyoifikia...Binafsi napendekeza kwanza ianze JF RAdio then baadae ndo ije JF TV na Newspaper...Hongereni sana na poleni kwa kazi hii ngumu mliyoifanya mpaka wakati huu
 
Pole na Hongereni.. Andahani tunawatakia mafanikio mema.

Kuhusu JF TV au radio ningependekeza kuwe na mtazamo au vision ya kuwalenga watu walio nje ya miiji zaidi.

Najua kiundeshaji na kiutekelezaji hili ni gumu lakini naomba iwepo vision/mission hiyo ili JF iwe unique na hayo magazeti,TV na radio nyingine. Lakini sio mbaya ukiw ana gazzeti linatoka mara 1ja kwa wiki au TV inatangaza mara 1ja kwa wiki lakini inakuja na habri ya mafaniko, matatizo , opprtunities zilizopo kijiji au wilaya fulani
 
Big up JF nawatakia mabadiliko na mafanikio mema na Mungu atawatangulia
 
Invisible and your company ,GOD bless you for what you are doing for this poor country!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom